IQNA

Njama za Wazayuni

Saudia yasema imemkamata raia wake aliyemuwezesha Yahudi Muisraeli kuingia Makka

19:54 - July 22, 2022
Habari ID: 3475522
TEHRAN (IQNA) –Saudi Arabia inasema imemkamata raia wake ya ambaye alimuwezesha mwandishi habari Yahudi Muisraeli kuingia katika mji mtakatifu wa Makka, jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwani wasio Waislamu hawaruhusiwi kuingia katika eneo hilo takatifu.

Polisi mjini Makka wamemfikisha mtuhumiwa huyo kwa Ofishi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma  baada ya kubainika kuwa alimsaidia Yahudi huyo  ambaye alikuwa akitumia pasi ya kusafiria ya Marekani kuingia katika mji mtakatifu wa Makka ,

Mnamo Ijumaa, msemaji wa polisi Makka alinukuliwa akitoa maelezo ya tuki  ambapo  mwandishi wa habari huyo Yahudi Muisraeli alitumia pasi ya Marekani kuingia Saudia na kusafirki hadi mji mtakatifu wa Makka kinyume cha sheria.

Msemaji huyo alibaini kuwa wote wanaotembelea Saudia wanapaswa kuzingatia na kuheshimu na kanuni zinazohusiana na misikiti mitakatifu nchini humo.

Katika video iliyorushwa kwenye akaunti yake ya mitandao yake ya kijamii, Gil Tamari mwandishi habari Muisraeli –Mmarekani na ambaye ni mhariri wa habari za kimataifa katika kanali ya televisheni ya  Channle  13 ya utawala wa Kizayuni wa Israel akiwa ndani ya gari akitembelea mji mtakatifu wa Makka hivi karibuni wakati wa msimu wa Hija wakati ambao ni kinyume cha sheria kwa wasiokuwa Waislamu kuingia katika mjin huo.

Katika baadhi ya picha, Tamari anaonekana akiwa katika Mlima Arafat, karibu na mji mtakatifu wa Makka, eneo ambalo hufanyika moja ya amali  muhimu zaidi za Hija.

Wasio Waislamu hawawezi kuingia katika mji mtakatifu wa Makka na baadhi ya sehemu za Madina.

Hayo yanajiri wakati ambao Saudi Arabia imekuwa ikitekeleza sera za makusudi za kujikurubisha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel jambo ambalo limewawezesha raia wengi wa Israel kuingia katika ufalme huo kwa siri.

Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel  hivi karibuni viliripoti kuwa, ndege maalumu ya shirika la ujasusi la utawala huo Mossad ilitua katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Shamoon Aaron, ripota wa chaneli ya televisheni ya utawala wa Kizayuni ya KAN 11 ameeleza katika ripoti kuwa, ndege ambayo hapo kabla ilikuwa ikitumiwa na Mossad, ilitua katika uwanja wa ndege wa mji wa mkuu wa Saudia, Riyadh.

3479787

captcha