IQNA

Al Kaaba Tukufu

Pazia la al-Kaaba (kiswa) labadilishwa siku ya kwanza ya Muharram + Video

15:38 - July 31, 2022
Habari ID: 3475561
TEHRAN (IQNA)- Jumamosi kumefanyika hafla ya kubadilisha pazia la al-Kaaba Tukufu linalojulikana kama Kiswa baada ya kuwadia mwezi wa Muharram 1444 Hijria, ambao ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu.

Wakuu wa Saudia mwaka huu wameakhirisha uvishaji pazia la Al Kaaba ambalo kawaida hubadilishwa 9 Dhul Hijja na badala yake wametekeleza shughuli hiyo tarehe Mosi Muharram.

Hii hapa klipu na picha za halfa hiyi ya kubadilisha pazia la Al Kaaba katika Msikiti Mtakatifu wa Makka. 

Kila mwaka pazia la hariri ambalo huwa limefunika al-Kaaba hubadilishwa na jipya kuwekwa. Hili ni pazia ambalo hutolewa hukatwa vipande vipande na kuzawadiwa wageni maalumu kutoka nchi za kigeni.

 

Kiswa ni pazia nyeusi ambayo hushonwa kwa hariri yenye uzito wa kilo 670 ambapo aya za Qur'ani hushonwa kwa uzi wa dhahabu katika pazio hilo.  Aya hizo hushindwa kwa dhahabu yenye uzito wa kilo 120 na uzi wa fedha wenye uzito wa kilo 100. Pazia ambalo huondolewa kukatwa vipande vipande na kutumwa katika nchi mbali mbali za Kiislamu kama zawadi kutoka kwa wakuu wa Saudia.

 

 

Kishikizo: AL KAABA ، MAAKA ، kiswa ، MUHARRAM
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha