Kwa mujibu wa taarifa , hafla ya makabidhiano ilihudhuriwa na Naibu Amir wa Mkoa wa Makkah pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hija na Umra. Mkataba rasmi wa makabidhiano ulisainiwa na Tawfiq Al-Rabiah, Mwenyekiti wa Urais Mkuu wa Masuala ya Msikiti Miwili Mitakatifu, pamoja na Abdul Malik bin Taha Al-Shaibi, mhudumu mkuu wa Kaaba.
Zoezi la kubadilisha Kiswa huanza rasmi katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kiislamu, 1 Muharram, ambayo mwaka huu inasadifiana na tarehe 27 Juni.
Kiswa hutengenezwa kila mwaka katika Kiwanda Maalum cha Mfalme Abdulaziz cha kutengeneza Kiswa ya Kaaba, kikitumia hariri asilia yenye rangi nyeusi ya hali ya juu. Kiswa huwa na urefu wa mita 14 na ukanda (hizam) mpana wa sentimita 95 ulioandikwa aya za Qur’ani kwa uzi wa dhahabu.
Ukanda huo hupita katika theluthi ya juu ya Kiswa na umeundwa kwa vipande 16 vinavyofikia urefu wa jumla wa mita 47.
Sherehe hii na ubadilishaji wa Kiswa ni sehemu ya urithi wa kiroho na kitamaduni wa Kiislamu unaozingatiwa kwa heshima kubwa kila mwaka mjini Makkah.
3493378