IQNA

Pazia la al-Kaaba (kiswa) labadilishwa + Video

18:19 - July 22, 2020
Habari ID: 3472988
TEHRAN (IQNA)- Sherehe imefanyika mjini Makka Jumapili kubadilisha pazia la al-Kaaba Tukufu linalojulikana kama Kiswa baada ya kuwadia mwezi wa Dhul Hija ambao ni mwezi wa kutekeleza Ibada ya Hija.

Kwa mujibu wa taarifa tovuti ya youm7, Ofisi ya Mkuu wa Msikiti Msikiti Mtakatifu wa Makka, al-Masjid al-Ḥaram na Msikiti Mtakatifu wa kama Al-Masjid an-Nabawi mjini Madina, imetoa taarifa kupitia ukurasa wa Twitter na kusema, kama ilivyo kawaida ya kila mwaka, pazia hilo limebadilishwa ikiwa ni katika kujitayarisha kwa ajili ya ibada ya Hija.

Kila mwaka pazia la hariri ambalo huwa limefunika al-Kaaba hubadilishwa na jipya kuwekwa katika siku ya 9 ya Dhul Hija.

Pazia ambalo hutolewa hukatwa vipande vipande na kuzawadiwa wageni maalumu kutoka nchi za kigeni.

Mwaka huu kutokana na janga la COVID-19 idadi ya Mahujaji imepungwa kwa kiasi kikubwa ambapo imekadiriwa kutakuwa na mahujaji wasiozidi 1000 tu kutoka ndani ya Saudia watakaojumuisha raia wa nchi hiyo na raia wa kigeni wanaoishi katika ufalme huo.

3911989/

Kishikizo: kiswa pazia kaaba hija
captcha