IQNA

Shughuli za Qur'ani

Shule ya Qur'ani ya Vijana yazinduliwa nchini Uturuki

20:17 - July 31, 2022
Habari ID: 3475564
TEHRAN (IQNA) - Hafla imefanyika Silopi, mkoa wa Sirnak, kusini mashariki mwa Uturuki, kuzindua shule ya kufundisha vijana kuhifadhi Qur'ani.

Idadi ya maafisa wa kidini, kitamaduni na kisiasa, akiwemo mkuu wa Kurugenzi ya Masuala ya Kidini (Diyanet) Ali Erbas, walihudhuria sherehe hiyo siku ya Ijumaa.

Shule ya Qur'ani ya Omar ibn Khattab ilizinduliwa katika jengo la orofa tano huko Silopi ambalo limewekwa vifaa tofauti vya kielimu na vingine.

Erbas katika hotuba yake alipongeza kufunguliwa kwa shule hiyo na kuelezea uzinduzi wa vituo vya Qur'ani kuwa ni miongoni mwa sherehe zenye thawabu zaidi.

Amesema kujifunza Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kufanyia kazi mafundisho yake na Sira ya Mtume Mtukufu (SAW), na kulea watoto na vijana kwenye njia ya Qur'ani na Sira kutapelekea kupatikana taifa lenye amani, furaha na umoja.

"Qur'an Tukufu inatualika katika matendo mema, umoja na kazi ya pamoja," aliongeza.

Erbas alielezea kuridhika kwa kuhudhuria sherehe hiyo na alitumai shule hiyo itakuwa chanzo cha baraka kwa kila mtu jijini.

Uturuki ni nchi ya Kiislamu katika eneo la baina Asia na Ulaya na takriban asilimia 99 ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu.

3479903

captcha