IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Nchi 49 zinashiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Uturuki

20:35 - October 02, 2022
Habari ID: 3475868
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 8 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Uturuki yanaendelea kwa kushirikisha wawakilishi kutoka nchi 49.

Mashindano hayo ya kimataifa yalianza katika mji wa mashariki wa Konya mnamo Alhamisi, Septemba 29.

Sherehe za ufunguzi zilihutubiwa na Ali Erbas, rais wa Kurugenzi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet).

Katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kunufaika na mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kuongeza kuwa ili kujenga mustakbali tunahitaji Kitabu hicho Kitukufu.

Erbas alisema Qur'ani inatofautisha ukweli na uwongo na kwamba ndio chimbuko la ukweli unaowafundisha wanadamu madhumuni ya kuumbwa.

Pia amewatakia mafanikio washindani wote na kusema ni aina ya mashindano ambayo hakuna walioshindwa.

Wahifadhi na wasomaji 63 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 49 wanachuana katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani.

Jopo la majaji hao linajumuisha wataalamu wa Qur'ani kutoka Uturuki pamoja na Algeria, Croatia, Yemen na Qatar.

Mashindano hayo yataendelea hadi tarehe 8 Oktoba na washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla itakayofanyika mjini Ankara, ambayo itahudhuriwa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Iran ina washindani wawili katika tukio la Qur'ani: Vahid Khazaei katika kategoria ya kisomo au qiraa na Hossein Khani katika kuhifadhi Qur'ani nzima.

4089112

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha