IQNA

Mkutano wa kimataifa wa Qiraa ya Qur’ani Tukufu wafanyika Istanbul, Uturuki

11:09 - November 07, 2017
Habari ID: 3471252
TEHRAN (IQNA)-Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu qiraa au usomaji wa Qur’ani Tukufu umefanyika katika mji wa Istanbul, Uturuki.

Wataalamu wanafikra na wasomi kutoka nchi mbali mbali duniani walihudhuria mkutano huo ulioanza Ijumaa iliyopita. Mkutano huo uliandaliwa na Idara ya Masuala ya Kidini katika Ofisi ya Rais wa Uturuki maarufu kama Diyanet.

Mkuu wa Diyanet Sheikh Ali Erbas, Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki na maafisa kadhaa wa ngazi za juu walihudhuria mkutano huo.

Akihutubu katika mkutano huo, Sheikh Erbas alisisitiza kuhusu nafasi muhimu ya sayansi ya qiraa ya Qur’ani Tukufu na kuongeza kuwa kunapaswa kufanyika jitihada zaidi katika uga huo.

Kongamano hilo la kimataifa ambalo lilimalizika Jumapili lililenga kujadili viwango vya qiraa ya Qur’ani Tukufu katika jamii za Waislamu duniani.

3660407/

captcha