IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Murtadi Rusdhie aliyeandika kitabu dhidi ya Uislamu ajeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa Marekani

12:40 - August 13, 2022
Habari ID: 3475616
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Salman Rushdie, mwandishi murtadi wa kitabu cha Aya za Shetani kinachomtusi na kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW, na ambaye ameshambuiwa kwa kuchomwa kisu mjini New York Marekani, ametangaza kuwa, baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua saa kadhaa, hivi sasa Rushdie anasaidiwa kuvuta pumzi kwa mashine ya kupumulia, lakini hawezi kuongea.

 Andrew Wylie, ameeleza kwamba, baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua saa kadhaa, sasa hivi Rushdie anasaidiwa kuvuta pumzi kwa mashine ya kupumulia, hata hivyo hana uwezo wa kuongea.

Wylie ameongeza kuwa, kuna uwezekano Rushdie akapoteza jicho lake moja, mishipa ya mkono wake imeharibiwa vibaya na kwamba kisu alichochomwa kimeliathiri vibaya ini lake pia. 

Salman Rushdie mwenye umri wa miaka 75, raia wa Uingereza na Marekani aliyeandika kitabu cha Aya za Shetani kinachomvunjia heshima Bwana Mtume SAW, alishambuliwa jukwaani hapo jana wakati alipokuwa akijiandaa kutoa mhadhara kusini magharibi ya jimbo la New York.

Polisi ya New York imetangaza kuwa, mtu aliyemshambulia Rushdie ametambuliwa kuwa ni Hadi Matar, kijana mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa New Jersey.

Hata hivyo taarifa ya polisi haijataja uraia wa mtuhumiwa huyo ambaye tayari amekamatwa na kuwekwa kizuizini na wala haijabainisha kama ana rekodi ya uhalifu au la.

Mwaka 1988, murtadi Salman Rushdie aliandika kitabu cha matusi cha Aya za Shetani, ambacho ndani yake kinamvunjia heshima Nabii Muhammad SAW. Kitendo hicho cha Rushdie kiliwakasirisha na kuwaghadhibisha mno Waislamu duniani.

Author of Blasphemous Anti-Islam Book Salman Rushdie Attacked in New York State

Author of Blasphemous Anti-Islam Book Salman Rushdie Attacked in New York State

 

3480061

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha