IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Murtadi Salman Rushdie apoteza jicho kufuatia shambulio

17:08 - October 24, 2022
Habari ID: 3475985
TEHRAN (IQNA)- Imedokezwa kuwa, murtadi Salman Rushdie aliyepata majeraha makubwa katika shambulio la mwezi Agosti sasa amepoteza uwezo wa kuona jicho lake moja huku mkono wake mmoja nao ukiwa umepooza.

Andrew Wylie ameliambia gazeti la lugha ya Kihispania la "El Pais" kwamba Rushdie, ambaye ana umri wa miaka 75, amepata madhara makubwa katika shambuliio la mwezi Agosti.

Amesema: "Rushdie amepoteza jicho moja... Alipata majeraha makubwa matatu shingoni mwake. Mkono mmoja umepooza kwa sababu mishipa kwenye mkono wake imekatwa. Na ana majeraha zaidi ya 15 kwenye kifua na mwilini mwake."

Wylie vile vile ameliambia gazeti hilo kuwa, kwa sasa hawezi kusema chochote kingine kuhusu aliko Salman Rushdie na hajui kama bado yuko hospitalini au amepelekwa sehemu nyingine.

Baada ya kuandika kitabu cha "Aya za Shetani" cha kuutukana Uislamu, murtadi Salman Rushdie, alipewa ulinzi mkubwa na madola ya kikoloni hasa Uingereza na Marekani kwa miaka mingi ili asishambuliwe. Hata hivyo alishambuliwa tarehe 12 Agosti mwaka huu wakati alipokuwa karibu kutoa mhadhara katika mjumuiko mmoja mjini New York Marekani.

Murtadi huyo aliwahishwa hospitalini baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye shambulio hilo lililokata mishipa ya mkono wake, kumjeruhi kwenye ini na kuumizwa vibaya jichoni. 

Shambulio hilo la tarehe 12 Agosti dhidi ya Salman Rushdie lilitokea miaka 33 baada ya Imam Khomeini MA mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutoa fatwa ya kuuawa murtadi huyo kutokana na kuutukana Uislamu kwa kutunga kitabu hicho cha Aya za Shetani.

Licha ya kampeni zake dhidi ya Uislamu, Rushdie alipewa tuzo ya heshima na Malkia Elizabeth II wa Uingereza mwaka 2008.

3480974

Kishikizo: salman rusdhie
captcha