IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Ayatullah Alireza Arafi alaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu Ujerumani

13:02 - August 13, 2022
Habari ID: 3475617
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Vyuo vya Kiislamu nchini Iran amelaani vikali kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Hamburg, Ujerumani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Ayatollah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Vyuo vya Kiislamu kote Iran, ametoa taarifa na kusema:

"Katika siku za maombolezo ya kiongozi wa mashahidi  Aba Abdillah al-Hussein, amani iwe juu yake, sio tu Mashia, bali pia  walioachwa huru na wampendao Imamu Hussein, amani iwe juu yake, kutoka katika kila madhehbu na dini duniani, wanaomboleza kifo cha kishahidi cha Mtukufu huyo na masahaba zake watukufu, watu wachache sana, walifanya kitendo kibaya na  kiovu cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu na Ahlul-Bayt, amani iwe juu yao, katika mji wa Hamburg."
Ayatullah Arafi ameongeza kuwa: Kitendo hiki kilifanyika huku kuheshimu matukufu ya dini kukiwa ni jambo la kisheria na linalokubalika katika jamii na sheria zote, na bila shaka kitendo hicho ambacho kinadhalilisha matukufu ya Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu hakitakuwa na matokeo mengine isipokuwa kueneza chuki na migawanyiko ya kidini.

Mkurugenzi wa Seminari za Kiislamu kote Iran amesema nukta ya kusikitisha katikak kitendo hicho kiovu, ambacho hakijawahi kutokea, ni kwamba kilitokea chini ya uangalizi na bila shaka ukimya na kutojali kwa polisi.
Ayatullah Arafi kwa kulaani kitendo hicho kiovu ambacho ni kinyume na mafundisho ya dini na tamaduni zote ametaka polisi na mfumo wa mahakama wa Ujerumani kuwafungulia mashitaka mashetani hao na kuzuia kukaririwa vitendo kama hivyo.
Kufuatia hatua ya kichochezi ya idadi ndogo ya wapinzani ya kuidhalilisha Qur'ani Tukufu na matukufu ya Kiislamu katika mji wa Hamburg, Balozi Mdogo wa Ujerumani mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na kukabidhiwa malalmiko rasmi ya Iran kuhusu kitendo hicho ambapo Iran imesisitiza kuwa wahusika wa hatua hiyo ya kukera wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.

https://www.iribnews.ir/fa/news/3539153

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha