IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Nchi 40 za Ulaya zashiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Ujerumani

20:54 - October 15, 2024
Habari ID: 3479600
IQNA - Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika Hamburg, Ujerumani, wiki iliyopita, yalihudhuriwa na washiriki 140 kutoka nchi 40 za Ulaya.

Jumuiya ya Msaada wa Kiislamu Duniani (OCII) iliandaa mashindano hayo kuanzia Oktoba 9 hadi 11.

Abdullah al-Sanan, mkuu wa kamati ya maandalizi, alisema washiriki walishindana katika kategoria tatu zinazojumuisha kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi nusu ya Qur'ani na kuhifadhi Juzuu tano za Qur'ani.

Amebainisha kuwa Msikiti wa Al-Noor mjini Hamburg ndio uliokuwa mwenyeji wa tukio hilo la siku tatu la Qur'ani.

Badr al-Samit, mkurugenzi wa OCII, amesema jumuiya hiyo iliandaa mashindano hayo kwa kuzingatia mtazamo wa kimkakati wenye lengo la kukuza utamaduni wa wastani wa Kiislamu.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jumuiya hiyo imetekeleza programu na miradi mbalimbali ya kuhudumia Qur'ani.

Ni pamoja na kuanzishwa na vifaa vya vituo 18 vya kuhifadhi Qur'ani katika nchi 6 ambavyo vimeweza kutoa mafunzo kwa wahifadhi zaidi ya 10,700 wa kiume na wa kike, aliongeza.

Aliendelea kusema kwamba OCII pia imesambaza zaidi ya nakala 84,000 za Qur'ani Tukufu zikiwemo baadhi ya nakala za Qur'ani kwa nukta nundu au Braille kwa wenye ulemavu wa macho, katika nchi 6.

40 European Countries Take Part in Germany’s Int’l Quran Contest  

40 European Countries Take Part in Germany’s Int’l Quran Contest  

4242496

captcha