IQNA

Kisa cha Manabii

Kisa cha Manabii wanne ambao dua zao zilijibiwa

22:07 - September 04, 2022
Habari ID: 3475734
TEHRAN (IQNA) - Kuna visa au hadithi nyingi katika Qur'ani Tukufu kuhusu Mitume ambazo zinaweza kusomwa kwa mitazamo tofauti. Moja ya vipengele ni jinsi manabii walivyozungumza na Mwenyezi Mungu na kubainisha maombi yao.

Qur'ani Tukufu inawataja mitume wanne waliomwomba Mungu kitu na dua yao ikakubaliwa.

Nabii wa kwanza hapa ni Nuhu. Aliwaita watu kwenye Tauhidi kwa takriban miaka 1,000 lakini hatimaye akawalaani huku wakiendelea kukataa mialiko yake: “Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. (Surah Ash-Shu'ara, aya ya 118) Mungu alikubali ombi hili. "Na (kumbukeni)  Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa.." (Surah Al-Anbiya, aya ya 76)

Nabii anayefuata ni Ayubu. Alipoteza familia yake na watoto na akawa mgonjwa sana kwamba hakuna mtu angemkaribia. “Na Ayubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu. (Sura Al-Anbiya aya ya 83)

Maombo haya yalijibiwa na Mwenyezi Mungu: “Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada." (Surah Al-Anbiya, aya ya 84)

Wa tatu ni Yona (Yunus). Pia anaitwa Dhul-Nun [maana yake halisi ni mmiliki wa samaki]. Yunus alizungumza na Mungu akiwa amenaswa ndani ya tumbo la samaki.

 “Na Dhul-Nun (Nabii Yunus) alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.  (Surah Al-Anbiya, aya ya 87) Alikiri kosa lake na akajuta kuwalaani wengine. " Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini. (Surah Al-Anbiya, aya ya 88)

Zakaria ndiye nabii wa nne katika kundi hili. Alikuwa shemeji yake Imran, baba yake Bibi Maryam (SA). Wote wawili Imran na Zakaria walikuwa wamezeeka na hawakuwa na watoto huku wake zao wakipenda kupata watoto. Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, mtoto mmoja alitunukiwa kila moja ya familia hizi. (Kumbukeni) alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.." (Surah Al-Imran, aya ya 35)

Ombi la mama yake Hazrat Maryam kutoka kwa Mungu lilimfanya Zakaria amuombe Mungu pia mtoto.

3480327

captcha