IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Iran yalaani chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa kidini katika nchi za Magharibi

22:55 - September 23, 2022
Habari ID: 3475828
TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia wa Iran amelaani uenezaji wa chuki dhidi ya Uislamu unaofanywa na baadhi ya nchi za Magharibi na vile vile ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya madhehebu ya dini za waliowachache, hususan Waislamu.

Akihutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 30 tangu kupitishwa kwa Tamko la Haki za Watu Waliowachache Kitaifa au Kikabila, Kidini na Kilugha, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisheria na kimataifa Reza Najafi ameashiria masiabu ya waliowachache kidini duniani kote. .

Kikao hicho kilifanyika kando ya kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Alhamisi jioni.

Najafi alibainisha kuwa anawakilisha nchi, ambayo inajumuisha tamaduni, dini, makabila na lugha tofauti, inayoongozwa na mafundisho ya kweli ya Uislamu na inaongozwa na historia ndefu ya kuvumiliana kati ya dini na kuishi pamoja kwa amani kati ya wafuasi wa dini za Ibrahimu.

Afisa huyo mkuu wa Iran amesisitiza kuwa, Wairani ni taifa moja bila kujali lugha na rangi zao.

Ameendelea kuashiria hatua zinazochukuliwa nchini Iran za kuhakikisha haki za watu walio wachache zinapatikana na kueleza kuwa, hatua za kulazimishana za upande mmoja na vikwazo vya kikatili vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani vimekuwa na taathira hasi na kuzua vikwazo katika njia ya kupatikana haki za watu.

Najafi alisisitiza kuwa kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kutendewa kwa utu na heshima.

"Hata hivyo, ulinzi wowote wa haki za walio wachache haupaswi kuingilia kati haki za kisheria na halali za nchi wanachama, pamoja na kanuni ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi, kama ilivyoelezwa katika tamko hilo," Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran amesisitiza.

"Sote tuna jukumu muhimu la kutoa fursa sawa kwa watu wa nchi yetu ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa, na kuzingatia sifa zetu bainifu katika sera, sheria na kanuni za kitaifa pamoja na maadili yote ya kitamaduni na maadili," Najafi alihitimisha.

3480595

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha