IQNA

Waislamu Marekani

Waislamu Marekani waendelea kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu baada ya 9/11

16:08 - September 12, 2022
Habari ID: 3475773
TEHRAN (IQNA) - Athari za baada ya mashambulizi yaSeptemba 11 za chuki dhidi ya Uislamu zinaendelea kuwakumba Waislamu Wamarekani huku ikiwa imetimia miaka 21 tokea mashambulizi hayo yajiri.

Kulingana na takwimu za  Idara ya Upelelezi ya Marekani, FBI, uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani uliongezeka mara tu baada ya Septemba 11, 2001, na bado unaendelea kuongezeka

"Waislamu wanaendelea kuwa walengwa wa chuki, uonevu, na ubaguzi kutokana na dhana potofu ambazo ziliendelezwa na watu wenye itikadi kali zinazodaiwa kuwa za Kiislamu katika miaka iliyofuata mashambulizi ya 9/11. Vyombo vya habari pia vimechangia hali hiyo" alisema Hussam Ayloush, mkurugenzi mtendaji wa Kitengo cha Los Angeles cha Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR).

"Miaka 21 baada ya mashambulizi, Waislamu wanaendelea kukabiliwa na tishio la ghasia."

Baada ya Septemba 11, Ayloush alisema, kulikuwa na "wimbi kali la  Marekani kutafuta adui."

"Ukweli wa kusikitisha ni kwamba kuna watu na mashirika ambayo yanafaidika kutokana na kuendeleza chuki dhidi ya Uislamu, ubaguzi na vita," alisema.

Chuki dhidi ya Uislamu au Waislamu - bado ni tatizo lililoenea nchini Marekani.

Zahra Jamal, mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Boniuk ya Chuo Kikuu cha Rice ya Kuvumiliana Kidini huko Houston, alisema asilimia 62 ya Waislamu wanaripoti kuhisi uadui unaotokana na dini na asilimia 65 walihisi kutoheshimiwa na wengine.

Alisema idadi inayohusiana na ubaguzi dhidi ya Waislamu inatisha na inaonyesha ni kwa kiasi gani chuki ya Uislamu imeongezeka nchini Marekani katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Ayloush alisema takwimu hizo hazishangazi kwa kuzingatia hali tete ya kisiasa nchini Marekani inayoendelezwa na Rais wa zamani Donald Trump katika kipindi chake cha uongozi.

"Urais wa Trump ulibadilika kuwa mtu mwenye chuki dhidi ya Uislamu. Alifanya ikubalike kijamii kuwa na chuki dhidi ya Uislamu,” alisema Ayloush.

Alibainisha kuwa Marekani ina historia ndefu ya "kudhalilisha na kuweka pembeni" makabila na wafuasi wa dini za wachache, wakiwemo Wenyeji wa Amerika, Waamerika wenye asili ya Afrika, na Waamerika wa Asia.

Njia pekee ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu baada ya 9/11 ni kushughulikia ana kwa ana na tatizo hilo, alisema.

"Ni muhimu kuwawajibisha watu wanaoendeleza ubaguzi wa rangi, ubaguzi na chuki dhidi ya wageni kwa maneno na vitendo vyao vya chuki katika sekta zote, iwe ni mpakani, kwenye uwanja wa ndege, kwa vyombo vya sheria, au kwa mwanasiasa," alisema Ayloush.

3480441

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani waislamu
captcha