IQNA

Jinai za Saudia nchini Yemen

Ripoti: Saudi Arabia imesababisha ukame na njaa nchini Yemen

11:26 - September 25, 2022
Habari ID: 3475836
TEHRAN (IQNA)- Shirika la Kimataifa la Kupambana na Mateso limesema katika ripoti yake kwamba, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ndio chimbuko la ukame na njaa inayowakabili wananchi wa Yemen kutokana na kuiziingira nchi nchi hiyo.

Shirika la Kimataifa la Kupambana na Mateso (World Organisation Against Torture) mbali na kulaani vitendo visivyo vya kibinadamu vya muungano huo dhidi ya Yemen limesema kuwa, hatua ya Saudia na washirika wake ya kuizingira nchi hiyo na kufanya mashambulio mtawalia ya anga yanayowalenga raia ni jinai ya wazi ya kivita.

Sehemu nyingine ya ripoti ya shirika hilo imebainisha kuwa, mzingiro wa Saudia na washirikak wake dhidi ya Yemen umekuwa kikwazo cha kufikishwa nchini humo bidhaa muhimu na za kimsingi ambazo zinahitajiwa na wananchi hao.

Shirika hilo limetoa mwito kwa jamii ya kimataifa hususan asasi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama kuchukua hatua za maana kuhitimisha mzingiro dhidi ya Yemen wa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia.

Mnamo Machi 2015 Saudi Arabia, kwa kushirikiana na Imarati na kwa uungaji mkono wa serikali ya Marekani, ilianzisha hujuma ya pande zote dhidi ya watu madhulumu wa Yemen ambao nchi yao ni masikini zaidi katika bara Arabu.

Vita hivyo ambavyo vimeshaua makumi ya maelfu ya watu vinaendelezwa sambamba na muungano huo wa Saudia kutekeleza mzingiro wa nchi kavu, baharini na angani dhidi ya Yemen na hivyo kuifanya nchi hiyo kukaribia kukumbwa na maafa ya kibinadamu. 

 

3480614

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha