IQNA

Hali ya Yemen

Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen: Maadui leo wako matatani

13:47 - September 02, 2022
Habari ID: 3475720
TEHRAN (IQNA) – Maadui wa Yemen wamo matatani kweli leo, amesema kiongozi wa harakati ya wananchi ya Ansarullah ya Yemen na kuongeza kuwa wameshindwa katika jaribio lao la kuikalia kwa mabavu nchi hiyo.

"Matarajio ya maadui kumiliki nchi yetu na kudhibiti watu wetu yanageuka kuwa mazigazi na hivyo wamekata tamaa...," Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi  alisema wakati wa hotuba Alhamisi.

"Adui leo yuko katika matatizo makubwa, watu wetu wanasimama upande wa jeshi lao, waaminifu na wamedhamiria kuzuia adui kuikalia nchi yetu," aliongeza.

Saudi Arabia ilianzisha vita vikali dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015 kwa ushirikiano na washirika wake wa Kiarabu na kwa msaada wa silaha, vifaa na kisiasa kutoka Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.

Lengo lilikuwa kuuweka tena utawala rafiki wa Riyadh wa rais wa zamani wa Yemen, Abd Rabbuh Mansour Hadi, na kuiponda Ansarullah, ambayo imekuwa ikiendesha masuala ya serikali bila kuwepo na serikali inayofanya kazi.

Wakati muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeshindwa kufikia malengo yake yoyote, vita hivyo vimeua mamia kwa maelfu ya Wayemeni na kuzua mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.

Makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa yalianza kutekelezwa mwezi Aprili kati ya muungano huo na Ansarullah. Makubaliano hayo yameongezwa mara mbili tangu wakati huo.

Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi  pia alitoa wito kwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia "kuchukua fursa ya uwekaji silaha na kusimamisha kabisa uchokozi wake."

“Tunautaka muungano  kuchukua fursa hiyo kusitisha kabisa uvamizi wake na kukomesha vizuizi na uvamizi, tunautaka muungano vamizi kujifunza mafunzo ambayo yamethibitisha malengo yake ya kuikalia kwa mabavu nchi yetu na kuwadhibiti watu wake ni jambi lisilowezekana ."

Itakumbukwa kuwa mwezi Machi 2015, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ziliongoza muungano vamizi wa nchi za Kiarabu katika kuanzisha mashambulizi ya kila upande dhidi ya nchi maskini ya Kiarabu ya Yemen kwa msaada na baraka kamili za Marekani na nchi za Ulaya kama ambavyo inaaminika pia kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel nao uko mstari wa mbele kuyasaidia kwa hali na mali madola hayo vamizi.

Tangu wakati huo hadi hivi sasa nchi hizo vamizi zimeizingira Yemen kutokea ardhini, majini na angani. Lakini wananchi wa Yemen kupitia jeshi lao na vikosi vya kujitolea vya wananchi maarufu kwa jina la Ansarulah, wameweza kusimama imara kuilinda nchi yao na kutoa pigo kubwa kwa wavamizi. 

3480311

Kishikizo: yemen ansarullah saudia
captcha