IQNA

Fikra za Kiislamu

Aya za Qur’ani Tukufu kuhusu ndoto za Mitume

13:32 - September 26, 2022
Habari ID: 3475842
Qur'ani Tukufu inataja kuota na athari zake kama suala muhimu, ikigusia juu yake katika aya kadhaa.

Marejeleo ya Qur’ani kuhusu ndoto za manabii, watawala, na watu wengine binafsi yanaonyesha uhusiano wa moja kwa moja kati ya ndoto na maisha ya watu na hadhi ya jamii.

Zifuatazo ni aya tatu za Qur’ani Tukufu zinazorejea ndoto za Mtume Muhammad (SAW). Bila shaka aya hizi hakika zinahitaji tafsiri zaidi ambazo zinapatikana katia vitabu maarufu vya Tafsiri za wanazuoni wa Kiislamu kama vile Tafsir al Mizan ya Allamah Tabatabai.

 “ Kumbuka alipo kuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache - na lau angeli kuonyesha kuwa ni wengi, mngeli ingiwa na woga, na mngeli zozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu kakuvueni. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua yalio vifuani.” (Surah Al-Anfal, aya ya 43)

 “Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na khofu. Yeye anajua msiyo yajua. Basi atakupeni kabla ya haya Ushindi karibuni." (Surah Al-Fath, aya ya 27)

 “Na tulipo kwambia (Ewe Muhammad): Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu. Na hatukuifanya ndoto tulio kuonyesha ila ni kuwajaribu watu, na mti ulio laaniwa katika Qur'ani. Na tunawahadharisha, lakini haiwazidishii ila uasi mkubwa.. (Surah Al-Isra', aya ya 60)

Hii  ni sehemu ya makala iliyoandikwa na Seyyed Mahmoud Javadi

3480571

captcha