IQNA

Taazia

Mwanachuoni wa Al-Azhar Afariki akiwa na umri wa miaka 74

17:59 - October 05, 2022
Habari ID: 3475883
TEHRAN (IQNA) - Sheikh Osama Abdel Azim, mwanazuoni wa Kiislamu na Qur'ani wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Maelfu ya Wamisri walihudhuria mazishi yake Jumanne, katika Msikiti wa Al-Muwasali katika eneo kusini mwa mji mkuu Cairo.

Wanazuoni na shakhsia wa kidini walituma risala za rambirambi baada ya kifo cha Sheikh Abdel Azim, ambaye alikuwa mkuu wa zamani wa idara ya teolojia katika kitivo cha mafundisho ya Kiislamu cha chuo kikuu hicho.

Walimuelezea kuwa ni mchamungu na mmoja wa waenezaji wakubwa wa Kiislamu ambaye alikuwa amejitolea sana hasa katika maudhui ya Sunnah ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Kwa mujibu wa Mohamed al-Saqir, waziri wa zamani wa Wakfu wa Misri, Sheikh Abdel Azim alijulikana kwa kutetea mbinu ya ufundishaji inayoegemezwa kwenye kuhimiza kuipenda Qur'ani Tukufu.

Alisema marehemu Sheikh aliamini kuwa kuhifadhi Kitabu kitukufu ni wajibu kwa Waislamu.

Alipata umaarufu miongoni mwa vijana pamoja na watu wazima kwa sababu ya hotuba zake rahisi na za kina ambazo ni rahisi kueleweka kwa makundi yote, ambazo zilienea sana kupitia tovuti za mawasiliano.

Sheikh Abdel Azim aliyezaliwa mwaka wa 1948, alikuwa na Shahada ya Uzamivu katika Fiqh (sheria ya Kiislamu) kutoka kitivo cha theolojia cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar.

4089837

Kishikizo: waislamu ، misri ، al azhar ، taazia ، Osama Abdel Azim
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha