IQNA

Mawaidha

Tutakabidhiwa Kitabu cha Amali Siku ya Kiyama

14:32 - November 16, 2024
Habari ID: 3479759
IQNA – Kitabu cha Amali tutakachopewa Siku ya Kiyama hakika si kama vitabu vya kawaida vilivyoandikwa kwenye karatasi, lakini, kwa mujibu wa baadhi ya wafasiri wa Qur’ani, ni nafsi zetu ambamo matendo yetu yote yamerekodiwa ndani yake.

Kutoka katika aya za Qur’an, pamoja na Aya ya 13 ya Sura Al-Isra, “Na kila mtu tumemfungia a´mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa.”

Inadokezwa  kuwa matendo yetu yote yameandikwa katika kitabu kwa usahihi wa hali ya juu na kwamba ikiwa mtu ni mchamungu, basi kitabu chake cha matendo atapewa kwa mkono wake wa kulia na ikiwa ni mwovu, kitabu chake cha matendo atakipokea mkono wake wa kushoto.

Baadhi ya wafasiri wa Qur'ani wamesema kuwa Kitabu cha matendo si chochote ila ni nafsi zetu ambamo ndani yake kumeandikwa matendo yetu yote, kwa sababu chochote tunachofanya kinaathiri nafsi zetu.

Kutajwa mara nyingi ya Kitabu cha Amali au matendo katika aya za Qur'an na Hadithi na msisitizo wa maandiko hayo matukufu juu ya ukweli kwamba maelezo yote ya matendo yetu, maneno na makusudio yetu yameandikwa ndani yake, inakusudiwa kutufanya tuweza waangalifu na tulipe umuhimu mazingatio kila tunachofanya  na kusema katika ulimwengu huu.

Mtu anayejua kwamba kamera inarekodi kila kitu anachofanya na kusema kwa faragha na hadharani, na kwamba rekodi siku moja zitaonyeshwa katika mahakama kuu ya haki, bila shaka atakuwa mwangalifu kuhusu tabia yake, mwenendo, na maneno na hivyo  Taqwa (ucha Mungu) itatawala ndani na nje ya uwepo wake.

Kuamini kuwepo kwa Kitabu cha Amali ambamo ndani yake kumeandikwa kila tendo, kubwa au dogo, kuamini kwamba kuna Malaika wanaofuatana nasi mchana na usiku na ambao ni wajibu wao kuandika tunayoyafanya, na kuamini kwamba Siku ya Kiyama Kitabu chetu cha Amali kitafunguliwa mbele ya kila mtu na dhambi zote tulizozitenda zitafichuliwa na tutaaibika mbele ya marafiki na maadui zetu, ni wazuiaji wa ajabu wa dhambi.

Pia, kujua kwamba kufunguliwa kwa Kitabu cha Amali ya wafanyao wema kutawafanya wawe na Fahari na furaha Siku ya Kiyama, ni mvuto wenye nguvu sana ya kutenda mema.

Ingawa imani juu ya kanuni hii ya Qur'ani (kuwepo kwa Kitabu cha Amali) inaweza kutosha kufundisha kila mtu haja ya kufanya matendo mema na kuepuka madhambi, wakati mwingine imani dhaifu na uzembe wa mtu mwenyewe humzuia kuzingatia ukweli huu.

3490646

captcha