IQNA

Njama dhidi ya Iran

CIA ni kinara wa majasusi ajinabi wanaoibua ghasia na kueneza ugaidi Iran

16:47 - October 29, 2022
Habari ID: 3476005
TEHRAN (IQNA)- Taarifa ya pamoja ya Wizara ya Intelijensia ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesema mashirika ajinabi ya kijasusi yakiongozwa na Shirika Kuu la Ujasusi la Marekani (CIA) yamekuwa na mchango mkubwa katika kupanga na kuratibu ghasia na fujo zilizoshuhudiwa hapa nchini kwa wiki kadhaa.

Taarifa hiyo imesema CIA ya Marekani ilikuwa imepanga mkakati mpana kwa ushirikiano na taasisi za kijasusi za waitifaki wa Washington wa kuvuruga usalama wa Iran, kufanya jinai dhidi ya Wairani na kukiuka mamlaka ya kujitawala taifa hili, hata kabla ya kuaga dunia Mahsa Amini.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Marekani ilitanga bajeti ya dola milioni 53 na kuyapa mashirika hayo ajinabi ya kijasusi ili kutekeleza amri na njama za Shirika Kuu la Ujasusi la Marekani (CIA) hapa nchini.

Taarifa ya pamoja ya Wizara ya Intelijensia ya Iran na IRGC imefichua kuwa, mashirika hayo ya kijasusi yanafanyakazi bega kwa bega na utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Ulaya ili kujaribu kutekeleza njama hizo ghalati, ambazo hata hivyo zimegonga mwamba.

Imesema maadui wa taifa hili wamepanga njia mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza 'vita vya vyombo vya habari' dhidi ya Iran, kupitia televisheni, tovuti za habari na mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo imefichua kuwa, baina ya Septemba 11 na Oktoba 12, mtandao wa kijamii wa Twitter uliruhusu kufunguliwa akaunti  feki 50,000 za lugha ya Kifarsi, zinazotumiwa kueneza propaganda na kusukuma mbele ajenda za maadui dhidi ya Iran.

Taarifa hiyo ilihitimisha kuwa licha ya juhudi zote hizo, maadui "walishindwa kufikia malengo yao waliyopanga," kwani "mradi wa kuiangamiza Iran umekabiliwa na kushindwa kwa kufedhehesha."

Ghasia zilizuka Iran baada ya Bi. Amini aliyekuwa umri wa miaka 22 kuanguka katika kituo cha polisi na kufariki akiwa anapata matibabu. Ripoti rasmi ya Idara ya Uchunguzi wa Maiti  ilisema kwamba kifo cha kutatanisha cha Amini kilisababishwa na ugonjwa aliokuwa nao kabla na si kwa kupigwa kichwa au viungo vingine muhimu vya mwili.

Machafuko hayo yamesababisha vifo vya makumi ya watu miongoni mwao wakiemo maafisa wa usalama na watu wasio na hatia huku baadhi ya watu wakihatarisha maandamano hayo kushambulia taasisi hiyo. Nchi nyingi za Magharibi zimeonyesha uungaji mkono wao kwa wafanya ghasia katika vitendo ambavyo Tehran inavitaja kuwa vya "kuchochea" ghasia na chuki.

4095092

Kishikizo: irgc CIA ghasia amini
captcha