IQNA

Njama dhidi ya Iran

Jibu la Rais wa Iran kwa Rais wa Marekani aliyetangaza kuunga mkono ghasia Iran

17:21 - November 04, 2022
Habari ID: 3476031
TEHRAN (IQNA)- Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya Rais Joe Biden wa Marekani ya kuunga mkono ghasia na machafuko nchini Iran na kusema, "Rais wa Marekani amedai kwamba "tuna mipango ya kuikomboa Iran"; hata hivyo anapaswa kuelewa kwamba Iran ilikombolewa miaka 43 iliyopita na haitatekwa tena na Marekani wala kuwa gombe la kukamuliwa maziwa."

Rais Raisi ameyasema hayo leo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa inayosadifiana na tarehe 4 Novemba.

Rais wa Iran ambaye alikuwa akihutubia hadhara kubwa ya waandamanaji mjini Tehran katika Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Ubeberu ameeleza kuwa, amesema kwamba, Marekani imekuwa mstari wa mbele katika vita na umwagaji damu na inaharibu maslahi ya mataifa mbalimbali ili kupata maslahi yake binafsi. 

Raisi amesema kuwa roho ya kibeberu na kiistikbari haioani na maneno na rai za wananchi. Ameashiria baadhi ya maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uzalishaji wa dawa, chanjo na masuala ya anga na kusisitiza kuwa: Vijana wa Iran ndio wanaoshika nafasi ya juu katika kanda hii na dunia, na msafara wa ustawi na maendeleo wa Iran hautadorora na kupungua kasi kwa vitisho na vikwazo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Nguvu ya Iran si katika makombora na uwezo wa kijeshi pekee, bali uwezo wake uko katika mahudhurio ya mamilioni ya watu katika maadhimisho ya siku ya leo tarehe 13 Aban katika nchi nzima ya Iran ya Kiislamu.

Kwingineko katika hotuba yake, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini taifa kubwa la Iran liliweka mapambano dhidi ya dhulma na ukoloni katika ajenda yake na kuongeza kuwa: "Hakuna mlingano unaoweza kufikiwa katika kanda ya Magharibi mwa Asia bila ya kupasishwa na Iran."

Halikadhalika ameeleza kuwa, hii leo mfumo unaotawala Marekani ndio nembo na dhihirisho la uistikbari na ubeberu na kusema: Marekani inaelewa vyema kwamba, Iran ina ushawishi katika kanda ya Magharibi mwa Asia na hakuna jambo linaloweza kufanyika katika eneo hilo bila ya ridhaa na mwafaka wa Iran.

Sayyid Raisi amekumbusha kuwa Iran ya Kiislamu ilichukua hatua ya kulinda eneo hili kutokana na shari ya vibaraka wa Marekani na kwamba Luteni Jenerali Hajj Qassem Soleimani amekuwa nembo ya mapambano dhidi ya ugaidi duniani. Ameongeza kuwa: "Yale mliyoyafanya kwa watu wa Afghanistan, Syria, Iraq, kanda hii na dunia kwa jina la uhuru yapo mbele ya macho yetu na tunaona hali ya nchi hizo na jinsi mnavyoyafanya mataifa mbalimbali kuwa watumwa na mateka wenu kwa kutumia jina la uhuru na kupigana na ugaidi; lakini mnapaswa kujua kwamba yale mliyoyafanya katika baadhi ya nchi kama vile Libya na Syria hamuwezi kuyatekeleza nchini Iran."

4096820

captcha