IQNA

Kanuni za Imani ya Kiislamu; Ufufuo /1

Je, wanadamu watatoweka kabisa baada ya kifo?

15:33 - November 16, 2022
Habari ID: 3476098
TEHRAN (IQNA) – Baadhi ya maswali ni ya ulimwengu wote na yapo katika akili ya kila mwanadamu. Mmoja kati ya maswali hayo ni kuhusu hatima yetu. Nini matokeo ya maisha na nini itakuwa hatima yetu? Hili limezungumziwa ndani ya Qur'ani katika fremu ya itikadi ya Ma’ad (Ufufuo).

Hakuna mtu ambaye hana maswali kuhusu yatakayotokea katika mustakabali wa mwanadamu na ulimwengu. Mwisho wetu utakuwa nini? Nini lengo na matokeo ya maisha? Maswali haya yapo katika akili ya kila mtu. Ndiyo maana dhana ya Ufufuo ina umuhimu mkubwa katika akili ya kila mtu na ni sehemu ya Fitra (au maumbile asili).

Neno Ma’ad linatokana na mzizi wa Auwd, ambalo linamaanisha kurudi na kufufuka tena, na linahusu maisha baada ya kifo. Baadhi ya thuluthi ya aya za Qur'ani Tukufu zinahusu Ma'ad na masuala yanayohusiana nayo.

Kuamini Ma’ad ni itikadi za kimsingi za Uislamu na kwa kuzingatia imani hii, matendo ya mtu yanatathminiwa Siku ya Kiyama na kisha analipwa au kuadhibiwa kwa mema au mabaya aliyoyatenda.

Kuna aina mbili za majibu kwa maswali yaliyotajwa hapo juu kuhusu hatima ya binadamu;

1- Imani zote za Mwenyezi Mungu, kwa kuzingatia sababu zitakazotajwa baadaye, zinazingatia mustakabali wa wanaadamu na ulimwengu na matokeo ya juhudi zao kuwa yenye nuru na yenye kuleta matumaini.

Qur'ani Tukufu inasema: “…Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. (Aya ya 42 ya Surah An-Najm)

2- Wenye itikadi zisizo na imani kwa Mwenyezi Mungu wanauona mustakabali wa ulimwengu na ubinadamu kuwa uliojaa giza, uharibifu na pia mwanaamini kuwa hatimaya mwanadamu atagonga mwamba na hakutakua na maisha baada ya maisha ya sasa duniani. Mtazamo huu ni hatari sana na wa kukata tamaa. Aidha, shule hizi hazina sababu za kisayansi kuthibitisha wazo hili.

Qur’ani Tukufu inasema: “Wanasema: ‘Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. (Aya ya 24 ya Surat Al-Jathiya)

Kukanusha huku hakutokani na hoja na uthibitisho bali ni msingi tu wa mfululizo wa hadaa iliyowagubika wakanushaji.

captcha