IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu / 35

Zijue Biashara zisizo na hasara katika Sura Fatir

20:43 - October 27, 2022
Habari ID: 3475994
TEHRAN (IQNA) - Mwanadamu anahitaji shughuli na kazi ili kupata pesa kwa ajili ya kuwa na maisha yaliyojaa amani na faraja. Qur'ani Tukufu imewaalika wanadamu kufanya biashara ambayo ndani yake hakuna hasara na ambayo inawapeleka kwenye amani ya milele.

Fatir ni jina la sura ya 35 ya Quran Tukufu. Ina Aya 45 na iko katika Juzuu ya 22. Fatir, ambayo ni Makki, ni Sura ya 43 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina lake linatokana na neno Fatir katika aya ya kwanza ya Sura. Fatir maana yake ni Muumba wa mbingu na ardhi. Pia inasemekana kumaanisha uumbaji bila utangulizi wowote na mifano iliyotangulia. Wengine wameitafsiri kama maumbile yenye ubunifu.

Surah Fatir inawaonya watu dhidi ya kudanganywa na mambo ya kidunia na vishawishi vya Shetani. Inaeleza watu kuwa wahitaji na Mungu kuwa hana haja.

Ili watu wamjue Mungu na Kumshukuru, Sura inataja baadhi ya neema walizopewa watu na Mwenyezi Mungu, ikiwa ni pamoja na mvua, kuchagua mume au mke, na kuwepo kwa bahari mbili, moja ya chumvi na yenye maji matamu zikiwa zinakaribiana bila maji kuchanganyika

Vile vile inazungumzia suala la kufufuliwa, baadhi ya vipengele vya Siku ya Kiyama, na majuto ya makafiri na kutaka kwao kurejea duniani ili kufidia makosa yao.

Katika baadhi ya aya zake, kusoma Qur'an, kuswali na kutoa sadaka kumetajwa kuwa ni biashara zisizo na hasara.

Maudhui ya Surah Fatir yanaweza kugawanywa katika sehemu tano:

Sehemu kubwa ya Aya ni kuhusu dalili za adhama ya Mwenyezi Mungu katika ulimwengu na sababu za Tauhidi.

Sehemu nyingine inazungumzia Tadbir au busara  ya Mwenyezi Mungu (inayoendesha dunia) na uumbaji wa mwanadamu kutokana na udongo na hatua za ukuaji wake.

Sehemu ya Sura inahusu ufufuo na matokeo ya Akhera ya matendo yetu hapa duniani.

Baadhi ya aya zinarejelea uongozi wa Manabii wa Mwenyezi Mungu na mapambano yao ya kuendelea dhidi ya maadui wakaidi.

Na sehemu ya aya za sura hii zinataja maonyo na maagizo ya Mwenyezi Mungu katika maeneo tofauti.

captcha