IQNA

Palestina

Uingereza yasisitiza haitauhamishia ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi Quds

19:20 - November 22, 2022
Habari ID: 3476131
TEHRAN (IQNA)- Kwa mara nyingine, Uingereza kutokana na mashinikizio na ukosoaji wa ndani na nje ya nchi, imesisitiza kuwa haina mpango wa kuuhamishia ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi katika mji wa Quds Tukufu (Jerusalem), huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel

Uingereza yasisitiza haitauhamishia ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi QudsHayo yalisemwa jana Jumatatu na Shailesh Vara, kiongozi wa ujumbe wa Bunge la Uingereza katika Jumuiya ya Kimataifa ya Mabunge (IPU) nchini Jordan, walipokutana na kufanya mazungumzo na Maseneta wa nchi hiyo ya Kiarabu mjini Amman.

Mbunge huyo wa Uingereza ameeleza bayana kuwa, nchi hiyo haina mpango wa kuuhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds tukufu kutoka Tel Aviv.

Ujumbe wa Jordan kwenye mazungumzo hayo uliongozwa na Seneta Hani Mulki, ambaye ameeleza bayana kuwa, Palestina itasalia kuwa kadhia kuu kwa ulimwengu wa Kiarabu.

Mapema mwezi huu, vyombo vya habari viliripoti kuwa serikali mpya ya Uingereza imelegeza kamba kuhusiana na mpango wa serikali ya waziri mkuu wa zamani Liz Truss wa kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.

Septemba 22, wakati Liz Truss alipokutana na waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Yair Lapid mjini New York pembeni ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, aliahidi kuwa London itauhamishia ubalozi wake katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.

Ahadi hiyo aliyotoa Truss kwa Lapid ilipokelewa na kuungwa mkono na viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na ikapingwa na kulaaniwa vikali na waungaji mkono wa Palestina katika nchi mbalimbali.

Msemaji wa Rishi Sonak alitangaza kuwa serikali ya waziri mkuu huyo mpya wa Uingereza haina mpango wa kuhamishia ubalozi wa nchi hiyo Quds tukufu inayokaliwa kwa mabavu.

3481365

captcha