IQNA

Kadhia ya Quds

Hamas yapinga vikali mpango wa Uingereza kuhamishia ubalozi wake mjini Quds

23:28 - September 24, 2022
Habari ID: 3475835
TEHRAN(IQNA)- Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameashiria mpango wa Uingereza wa kuuhamisha ubalozi ulioko Tel Aviv hadi Quds Tukufu(Jerusalem) na kueleza kuwa: hatua hiyo haibadili kivyovyote uhakika wa kihistoria.

Gazeti la Telegraph la Uingereza limezinukuu duru za kuaminika na kuripoti kuwa, katika mazungumzo kati yake na Yair Lapid Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Liz Truss Waziri Mkuu wa Uingereza amegusia uwezekano wa nchi hiyo kuhamishia ubalozi wake huko Quds, mji wa Kipalestina ambao hivi sasa unakaliwa kwa mabavu na  utawala haramu wa Israel.

Abdul Latif al Qanou Msemaji wa harakati ya Hamas alieleza kuwa, nia ya Uingereza ya kutaka kuhamishia ubalozi wake huko Quds inadhihirisha upendeleo wa wazi kwa utawala wa kikoloni wa Israel lakini kitendo hicho hakiwezi kubadili  kivyovyote uhakika wa kihistoria.   

Al Qanou ameongeza kuwa Uingereza siku zote inawaunga mkono ghasibu wa Israel unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu; na nchi hiyo ndiyo iliyowaahidi Wazayuni ardhi ya Wapalestina; kwa hiyo kuhamishiwa ubalozi huo pia kunafanyika katika fremu ya kuendeleza uadui na chokochoko dhidi ya matukufu ya Kiislamu na Kikristo.  

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina amesema: Quds ni ardhi iliyoghusubiwa na kukaliwa kwa mabavu na ni haki ya wananchi wa Palestina. Hatua hiyo ya Uingereza inamaanisha kuwa bega kwa bega na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.

4087303

Kishikizo: hamas ، palestina ، uingereza ، quds tukufu ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha