IQNA

Kujifunza Qur'ani

Mwalimu wa Misri asema watoto waanze kujifunza Qur’ani wakiwa wadogo

20:46 - September 25, 2022
Habari ID: 3475839
TEHRAN (IQNA) - Sheikh Mohamed Ata al-Basyuni ni mwalimu wa Qur'ani mwenye umri wa miaka 85 katika mji mmoja mkoani Gharbia nchini Misri.

Sheikh Basyuni ametumia takriban miaka 70 ya maisha yake kuwafundisha watoto Qur'ani.

Anasema watoto wanapaswa kuanza kujifunza Quran wakiwa wadogo, na kuongeza kuwa miaka mitano ni umri mzuri wa kuanza kuhifadhi Kitabu hicho Kitukufu.

Katika umri huu, chochote ambacho watoto hujifunza hubaki akilini mwao na hivyo kuhifadhi ni rahisi kuliko miaka ya baadaye, anasema.

Basyuni mwenyewe alianza kujifunza Qur’ani akiwa na umri wa miaka minane kwa kuhimizwa na babu yake.

Aliweza kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu baada ya miaka miwili.

Katika kipindi cha miaka 70 iliyopita, amefundisha Qur'ani kwa watoto katika moja ya vyumba vya nyumba yake.

Wengi wa wale waliohifadhi Quran kwa kuhudhuria darsa zake sasa wamekuwa walimu wa Qur’ani, wahubiri, na wasomi wa vyuo vikuu.

Qur’ani Tukufu ndio Maandiko pekee ya kidini ambayo yanahifadhiwa kikamilifu na wafuasi wake.

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Quran ina Juzu (sehemu) 30, Sura 114 na aya 6,236.

 4087662

captcha