IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /20

Ahmed Al-Reziqi; Qari mbunifu katika mtindo wa qiraa ya Ustadh Minshawi

16:37 - January 21, 2023
Habari ID: 3476440
TEHRAN (IQNA) – Ahmed al-Reziqi alikuwa qari kutoka kusini mwa Misri ambaye alishawishiwa sana na Abdul Basit Abdul Samad na Mohamed Sidiq Minshawi lakini pia alikuwa na ubunifu na weledi katika usomaji wa Qur'ani.

Ahmed Shahat Ahmed al-Reziqi alizaliwa mwaka 1938 katika kijiji cha Reziqat katika Jimbo la Qena nchini Misri.

Alikuwa miongoni mwa wale wa kizazi cha tatu cha wasomaji Qur'ani wa Misri. Alipata umaarufu baada ya magwiji kama Abdul Basit Abdul Samad, Mohamed Sidiq Minshawi na Mustafa Ismail.

Alikuwa rika la Ragheb Mustafa Ghalwash na Abdul Aziz Hassan.

Al-Reziqi aliathiriwa na kufuata mtindo wa Minshawi, mtindo ambao umekuwa wa kawaida kusini mwa Misri.

Yeye, hata hivyo, alikuwa na ubunifu na weledi wake katika qiraa au usomaji Qur'ani Tukufu.

Visomo vichache vya Al-Reziqi vimesalia leo kwa sababu hakupenda sana kusoma Qur'ani Tukufu katika vikao vya umma ambavyo kawaida qiraa hurekodiwa.

Mitindo ya usomaji au qiraa  ya Qur'ani inaweza kugawanywa katika vikundi vitatu: hai, iliyotoweka na kongwe. Mitindo hai ni ile ambayo imekuwa na mashabiki wengi kila wakati. Iliyotoweka ni ile ambayo wachache hupenda na kusahaulika hatua kwa hatua. Mitindo ya zamani au mkongwe ni ule unaojumuisha ubunifu fulani na huwa na  wafuasi wasiowengi wengi. Mtindo wa usomaji wa Al-Reziqi unaweza kuainishwa kama wa tatu.

Kinachofuata ni kisomo chake cha aya ya 17-35 ya Surah Taha:

captcha