IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /17

Mohammed Ahmed Omran; Qari aliyebuni mtindo wake mwenyewe katika Ibtihal

11:49 - January 15, 2023
Habari ID: 3476407
TEHRAN (IQNA) – Mohammed Ahmed Omran alikuwa qari mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka Misri na msomaji wa Ibtihal (usomaji dua unaoshabihiana na qiraa ya Qur’ani Tukufu).

Alipata upofu katika umri mdogo lakini kutokana na dua ya mama yake, akawa Msomaji Qur’ani Tukufu anayetambulika duniani.

Mohammed alizaliwa mwaka 1944 katika mji wa Tahta katika Jimbo la Sohag nchini Misri.

Baada ya kupoteza macho yake, mama yake alimiomba Mwenyezi Mungu kwamba amsaidie mwanae kuwa mhifadhi na msomaji wa Qur’ani Tukufu. Dua ya mama ilikubaliwa na Muhammad aliweza kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 10.

Pia alijifunza kanuni za usomaji na sheria za Tajweed akiwa na umri wa miaka 12 na akapokea idhini au ijaza ya kusoma Qur’ani Tukufu.

Mohammed alishawishiwa sana na Sheikh Naqshbandi (1920-1976) ambaye alimtaka aende Cairo na alifanya hivyo. Huko Cairo, alienda katika shule ya kasida maalumu kwa wenye ulemavu wa macho na aliosoma fani ya Maqamat.

Baada ya kuhitimu kutoka shule ya upili, Mohammed alianza kufanya kazi katika kampuni ya uigizaji. Pia alisoma Qur’ani Tukufu na kuimba qasida kwenye msikiti wa kampuni hiyo.

Aliingia kwenye njia ya umaarufu baada ya kufaulu katika mtihani wa kujiunga na Redio ya Qur'ani ya Misri kama msomaji wa Ibtihal.

Kuanzia hapo na kuendelea, alihudhuria programu nyingi za kidini na sherehe za kusoma Ibtihal.

Muhammad alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika usomaji wa Qur’ani Tukufu nchini Misri.

Aidha alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kusoma Qur’ani Tukufu na Ibtihal katika sherehe.

Mohammed Ahmed Omran alifariki Oktoba 6, 1994 kabla ya kufikisha umri wa miaka 50.

Huu hapa usomaji wake wa aya ya 3 ya Surah Fatir:

Ifuatayo ni faili la sauti la mmoja wa Ibtihal zake katika mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW).

 

captcha