IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Qur’ani Tukufu yavunjiwa heshima Uholanzi baada ya Uswidi

21:45 - January 24, 2023
Habari ID: 3476456
TEHRAN (IQNA) – Baada ya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Uswidi mwishoni mwa juma, kulikuwa na kitendo kingine cha kufuru kilichotekelezwa na mmoja wa vinara wa harakati za chuki dhidi ya Uislamu Ulaya, wakati huu nchini Uholanzi.

Kinara wa Uholanzi wa kundi la siasa kali za mrengo wa kulia, Wazalendo Wazungu Wanaopinga Uislamu katika Ulimwengu wa Magharibi (PEGIDA), amevunjia heshima  nakala ya Qur’ani Tukufu nchini Uholanzi, akitishia kuzidisha hali ya wasiwasi iliyoibuka kufuatia tukio sawa na hilo dhidi ya Qur’ani  nchini Uswidi (Sweden).

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu ilionyesha mchochezi mwenye chuki dhidi ya Uislamu Edwin Wagensveld akiichana Qur’ani Tukufu kabla ya kuiteketeza moto.

Baada ya kukamatwa mara mbili zilizopita kwa sababu ya shughuli zake dhidi ya Uislamu, Wagensveld alidai kwenye video hiyo kwamba alipokea kibali kutoka kwa mji wa The Hague kwa ajili ya "kuharibu Qur’ani."

"Haki ya kuandamana na haki ya uhuru wa kujieleza ni haki za binadamu na uhuru zinazolindwa kikatiba na mkataba," ilisema barua ya Meya wa The Hague Jan van Zanen.

Lakini iliongeza kuwa "kimsingi kuchoma vitu hakuruhusiwi, kwa sababu hii inaweza kusababisha hatari."

Kipande cha video kisha kinaonyesha Quran na kurasa zake zilizochanika zikiwaka moto katika kitu kinachofanana na kikaangio kilichowekwa kwenye sakafu.

“Watu wanaotujua na wanaotufuatilia wanajua hatukati tamaa, tusikubali kutishwa na vurugu na vitisho vya kuuawa,” alisema mzungu huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu.

Kitendo hicho kumekuja siku chache tu baada ya tukio jingine la kuchomwa moto nakala ya Qur’ani Tukufu nchini Uswidi siku ya Jumamosi, ambalo lilizusha shutuma na maandamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kiongozi wa chuki dhidi ya Uislamu Rasmus Paludan alitekeleza kitendo hicho kiovu mbele ya Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm baada ya kupata kibali kutoka kwa serikali ya Uswidi.

3482193

captcha