IQNA

Kadhia ya Palestina

Qatar yasisitiza kuunga mkono ukombozi wa Palestina

23:06 - January 25, 2023
Habari ID: 3476463
TEHRAN (IQNA) - Balozi wa Qatar katika Umoja wa Ulaya na muungano wa kijeshi wa NATO amesisitiza uungaji mkono wa nchi yake kwa ukombozi wa Palestina.

Abdulaziz bin Ahmed Al Malki alishiriki katika mkutano wa Mabalozi na wakuu wa balozi za Kiarabu mjini Brussels na Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh na Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al Malki, kwa mwaliko wa ujumbe wa Palestina katika Umoja wa Ulaya. .

Katika hotuba yake wakati wa mkutano huo, mwanadiplomasia huyo alisisitiza msimamo thabiti wa Qatar kuhusu kadhia ya Palestina, haki halali za watu ndugu wa Palestina, na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina kwenye mipaka ya 1967 na al-Quds ukiwa mji mkuu wake. .

Vile vile amerejelea msimamo wa Qatar wa kulaani hujuma za mara kwa mara za Israel dhidi ya  Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Al Quds (Jerusalem), na kusema huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Aidha amesema Qatar inataka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha sera ya kimfumo ya Israel ya kueneza uchokozi dhidi ya watu wa Palestina na ardhi zao na matakatifu ya Kiislamu na Kikristo.

Amesema Qataritanedelea kutoa misaada ya kibinadamu, na maendeleo ya Qatar kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, hasa wale ambao wanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na maisha iliyosababishwa na mzingiro wa Israel dhidi ya ukanda huo.

3482213

Kishikizo: qatar palestina israel
captcha