IQNA

Diplomasia

Rais wa Iran: mashine ya vita ya utawala wa Kizayuni izuiwe isiendeleze jinai na mauaji ya kimbari

22:08 - October 29, 2023
Habari ID: 3477809
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo ya simu aliyofanya na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad bin Khalifa Al Thani kwamba, leo taifa la Palestina linahitaji zaidi uungaji mkono athirifu wa walimwengu na hasa wa nchi za Kiislamu kuliko wakati wowote ule.
Katika mazungumzo hayo waliyofanya Jumamosi, viongozi hao  wameshauriana juu ya hatua za kivitendo zinazopasa kuchukuliwa kwa ajili ya kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.
 
Rais Raisi amesema, uungaji mkono wa nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kwa utawala wa Kizayuni ni sawa na kutoa baraka nchi hizo kwa utawala huo ghasibu za kufanya jinai dhidi ya Wapalestina wa Gaza na akabainisha kuwa: "leo taifa la Palestina linahitaji zaidi uungaji mkono athirifu wa walimwengu na hasa wa nchi za Kiislamu kuliko wakati wowote ule ili kuizuia mashine ya vita ya utawala wa Kizayuni isiendeleze jinai na mauaji ya kimbari."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa la jinai za utawala wa Kizayuni katika kuua wanawake na watoto wa Kipalestina, sambamba na kusababisha hali mbaya ya kibinadamu kwa kukata maji na umeme na kuzuia kuingizwa chakula na dawa huko Gaza; na akasisitizia ulazima wa nchi za Kiislamu kuchukua msimamo thabiti, wa pamoja na wa wazi katika kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.

Kwa upande wake, Amir wa Qatar amesema, matukio yanayojiri leo huko Gaza ni ushahidi wa siasa na sera za undumakuwili na za kuaibisha za nchi za Magharibi na akasisitiza kuwa: "zikiwa na umoja, nchi za eneo na nchi za Kiislamu zinaweza kuisimamisha mashine vita ya utawala wa Kizayuni."
 
Amir wa Qatar amesitiza pia kuhusu msimamo wa nchi yake wa kuunga mkono haki za taifa la Palestina katika kujiamulia hatima na mustakabali wake na akasema: utawala wa Kizayuni umekiuka sheria na taratibu zote za kimataifa za kiutu na wala haujali kutenda jinai yoyote ile.
4178345
Habari zinazohusiana
captcha