IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /27

Qari aliyeisoma Qur'ani Tukufu kwa ubora hata akiwa na umri wa miaka 88

22:35 - February 12, 2023
Habari ID: 3476550
TEHRAN (IQNA) – Ahmed Mohamed Amer alikuwa qari mashuhuri wa Misri ambaye alisoma Qur’ani Tukufu kwa ubora na kwa sauti maridadi hata alipokuwa na umri wa miaka 88.

Ahmed alizaliwa katika familia ambayo watu wake walikuwa ni wahifadhi na wasomaji wa Qur’ani  Tukufu. Baba yake alikuwa msomaji maarufu wa Qur’ani na babu yake alikuwa hafidh wa  Qur’ani Tukufu.

Ahmed alizaliwa Misri mwaka wa 1927, alianza kujifunza  kuhifadhi Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 4 na akawa hafidh na miaka 11.

Akiwa na umri wa miaka 13 alijifunza kanuni za usomaji na Tajweed na alisoma Qur’ani Tukufu kwa urahisi. Watu katika kijiji chake walimwita Ustadh akiwa na umri wamiaka 13 na waliendelea kumuita hivyo hadi kifo chake.

Awali alifuata mtindo wa qiraa wa Sheikh Abdul Fattah Sha’shaei.

Mnamo 1956, alifaulu mtihani wa kuingia katika Idhaa ya Misri lakini hivi baada ya muda usio mrefu idhaa hiyo wakati huo ilifungwa kwa muda kutokana na vita na hatimaye alianza  usomaji wake katika Idhaa ya Misri mnamo Novemba 1963.

Ziara ya kwanza ya Ahmed katika nchi ya kigeni ilikuja mwaka 1958 aliposafiri hadi Sudan pamoja na Khalil al-Husary na Abdul Hakam mwaka wa 1958.

Baadaye alisafiri kwenda nchi zingine kama India, Yemen, Iran, Bahrain na Syria kwa ajili ya kushiriki katika vikao vya usomaji wa Qur'ani Tukufu.

Ahmed Mohamed Amer alikuwa na sauti moja yenye nguvu zaidi miongoni mwa wasomaji Qur’ani nchini  Misri katika zama zake. Angeweza hata kusoma Quran kwa nguvu kamili akiwa na umri wa miaka 88.

Ama kuhusu mtindo, hakuwa na mtindo unaojitegemea na alifuata mtindo wa kisomo wa Abdul Fattah Sha’shaei na kisha Mustafa Ismail.

Klipu ifuatayo inaonyesha usomaji wake wa aya za Sura Al-Baqarah:

 

captcha