IQNA

Qurani Tukufu

Wasichana wa waliohifadhi Qur’ani Misri waenziwa

17:29 - March 08, 2023
Habari ID: 3476677
TEHRAN (IQNA) – Sherehe ilifanyika katika mji wa Giza, Misri, kwa ajili ya kuwaenzi wasichana ambao wamejifunza Qur’ani Tukufu kwa moyo kikamilifu.

Kituo cha kufundisha Qur'ani cha Al-Izz chenye uhusiano na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar kiliandaa hafla hiyo, ambayo pia ilihudhuriwa na wanazuoni wa Al-Azhar.

Wasichana hao walipokea vyeti vya heshima na vyeti vya kuhifadhi Quran katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu, ikiwa ni pamoja na wanafamilia wa wasichana.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walipongeza kuandaliwa kwa matukio kama haya ili kuhimiza uhifadhi wa Kitabu Kitukufu, wakisema wasichana hawa ambao wamejifunza Qur'ani kwa moyo ni hifadhi ya kimkakati ya Misri katika kukabiliana na upotovu..

Qur’ani Tukufu ndio Maandiko pekee ya kidini ambayo yanahifadhiwa kikamilifu moyoni na wafuasi wake.

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Quran tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Quran ina Juzuu (sehemu) 30, Sura 114 (sura) na aya 6,236.

Misri ni nchi ya Kiarabu katika Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 96.

Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani zimeenea sana sana katika nchi hiyo ya Kiarabu na Kiafrika yenye idadi kubwa ya wasomaji Qur’ani.

 

4126944

Habari zinazohusiana
Kishikizo: misri qurani tukufu
captcha