IQNA

Ushirikiano wa Kiislamu

Mapatano ya ushirikiano baina ya Kituo cha Utamaduni cha Iran na Radio ya Kiislamu ya Uganda

20:58 - April 03, 2023
Habari ID: 3476807
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda, kimetia saini mkataba wa maelewano (MoU) na Idhaa ya Kiislamu ya Bilal ya nchi hiyo ya kuhusu ushirikiano katika nyanja za kitamaduni.

Abdollah Abbasi, Mwambata wa Utamaduni wa Iran, na Faruq Walumanga, mkurugenzi wa Idhaa ya Kiislamu ya Bilal, walitia saini hati hiyo wakati wa mkutano katika kituo hicho.

Abbasi alisema katika mkutano huo kuwa pande hizo mbili zilikuwa na ushirikiano mzuri kabla ya kuzuka kwa janga la coronavirus na kwa kuwa sasa janga hilo limepungua, wanaweza kuinua kiwango cha ushirikiano tena.

Aidha ameashiria kampeni ya propaganda dhidi ya Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayofanywa na nchi za Magharibi na akasisitiza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha umma na kuzuia upotoshaji wa ukweli.

Kwa upande wake Walumanga alielezea matumaini yake kuwa ushirikiano wa kitamaduni utaimarishwa kati ya kituo hicho cha redio na kituo cha Iran.

Vile vile amesisitiza haja ya kusambaza habari sambamba na kuzingatia ukweli na haki za Kiislamu.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, Kituo cha Utamaduni cha Iran kitatayarisha vipindi, ikiwa ni pamoja na kipindi cha kila wiki kiitwacho "Amani kwa Mtazamo Mmoja", ambacho kitatangazwa kwenye Idhaa ya Kiislamu ya Bilal ya nchi hiyo.

3483042

captcha