IQNA

Elimu

Msomi mashuhuri wa Masomo ya Kiislamu Wilferd Madelung ameaga dunia

8:07 - May 11, 2023
Habari ID: 3476986
TEHRAN (IQNA) – Profesa mashuhuri wa masomo ya Kiislamu Wiferd Madelung alifariki dunia tarehe 9 Mei 2023.

Wilferd Madelung alizaliwa mnamo Desemba 26, 1930, huko Stuttgart, Ujerumani. Alimaliza elimu yake ya msingi na sekondari hapo kisha akahamia Chuo Kikuu cha Cairo, ambako alipata Shahada ya Awali (B.A.) katika Historia na Fasihi ya Kiislamu mnamo 1953.

Aliendelea na elimu yake ya juu nchini Ujerumani na kupata Shahada ya Uzimavi au  PhD ya Masomo ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Hamburg mwaka wa 1957. Tasnifu yake ilisimamiwa na wasomi wa Kiislamu wa Ujerumani R. Strothmann na B. Spuler. Alifanya kazi kama mshiriki wa kitamaduni wa Ujerumani Magharibi huko Baghdad kwa miaka mitatu (1958 - 1960) na kisha akajitolea maisha yake ya kitaaluma kwa Masomo ya Kiislamu. Profesa Madelung amekuwa na nafasi muhimu katika kuarifisha Ushia katika duru za Kiakademia barani Ulaya,

Amechangia pakubwa katika kuendeleza elimu kuhusu fikra na historia ya Kiislamu, hususan madhehebu ya Shia, kwa kuandika na kuhariri takriban vitabu 200 na makala katika majarida ya utafiti na encyclopedia na kuhakiki na kutambulisha vitabu 160. Kazi zake zinashughulikia mada mbalimbali kama vile theolojia, historia, fiqh, madhehebu za Kiislamu, wasifu na bibliografia. Baadhi ya kazi zake zimetafsiriwa kwa Kiajemi.

Moja ya kazi zake kuu ni “Urithi wa Muhammad (SAW)”, ambayo inaafikiana na mtazamo wa madhehebu ya Shia kuhusu nani angepaswa kumrithi Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Katika kitabu chake, Madelung anazungumzia mtazamo wa Qur'ani Tukufu kuhusu  urithi wa Mtume Muhammad SAW. Anasema kwamba Qur'ani Tukufu haina aya iliyo wazi juu ya suala hili, lakini ina mapendekezo mengi kuheshimu Ahul Bayt (AS) yaani watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (SAW).

 “Mienendo ya Kidini katika Iran ya Mapema ya Kiislamu”, “Harakati za Kidini na Kikabila katika Uislamu wa Zama za Kati”, “Uzushi wa Kiismaili”, “Kuja kwa Wafatimiya: Shahidi wa Kishia wa Kisasa”, na “Shule ya Kidini na Madhehebu katika Uislamu wa Zama za Kati” ni miongoni mwa vitabu vyake.

Alikuwa Profesa Mshiriki (1966-68) na kisha Profesa wa Historia ya Kiislamu kutoka 1969 hadi 1978 katika Chuo Kikuu cha Chicago kabla ya kukaimu kama Profesa wa Laudian wa Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Oxford kutoka 1978 hadi 1998.

4139848

captcha