IQNA

Uislamu ni chaguo langu

Nigeria: Mbulgaria aliyesilimu akamilisha somo la Qur'ani Tukufu

16:07 - December 06, 2023
Habari ID: 3477993
KANO (IQNA) - Mwanamke wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 62, Liliana Mohammed, amefikia ndoto yake ya kujifunza Qur'ani Tukufu katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria ambako amekuwa akiishi kwa zaidi ya miaka 30.

Bibi Mohammed, ambaye alisilimu takriban miaka 10 iliyopita, alisema Qur'ani Tukufu ni mwongozo wa maisha yake na kwamba amepata amani na utulivu katika Uislamu. Ameongeza kuwa:  “Uislamu umenipa amani, Qur'ani Tukufu pia ni mwongozo wangu. Ninaposoma Qur'ani Tukufu , ninahisi amani akilini mwangu,” alisema.

Aliolewa na mfanyabiashara wa jamii ya Hausa, marehemu Ibrahim Sambo, huko Bulgaria na kuhamia Kano pamoja naye. Walibarikiwa kupata watoto wawili, ambao pia ni Waislamu.

Bibi Mohammed alisema alianza elimu yake ya Qur'ani Tukufu akiwa nyumbani, kwa msaada wa mwalimu wa kike aliyemfundisha alfabeti za Kiarabu na jinsi ya kusoma Qur'ani kwa lugha ya Kiarabu.

Alisema aliendelea kutoka aya hadi aya, na sura hadi sura na hatimaye alihitimu kutoka Shule ya Kiislamu ya Mamba'irrahman huko Kano siku ya Jumamosi, pamoja na wanafunzi wengine watatu.

Alisema pia anahifadhi Qur'ani Tukufu, licha ya uzee wake.

Bibi Mohammed alisema anafurahia kuishi Kano, jimbo lenye Waislamu wengi, ambapo anaweza kutekeleza mafundisho ya Uislamu chini ya mazingira yanayofaa. Alisema nyakati Sala na Saumu nzuri  ikilinganishwa na sehemu zingine za ulimwengu.

Binti yake, Hamida Sambo, alimsifu mama yake kwa kuwalea vizuri na kuwaruhusu kufuata Uislamu kama marehemu baba yao. Alisema mamake amewafundisha kuwa watu wema katika jamii.

3486307

Kishikizo: uislamu Bulgaria
captcha