IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /80

Surah Abasa; Maelezo ya Siku wakati watu watakimbiana

16:30 - May 28, 2023
Habari ID: 3477058
TEHRAN (IQNA) – Kuna aya nyingi ndani ya Qur’an pamoja na Hadithi kuhusu maisha ya baada ya kifo na Siku ya Kiyama, zikiwemo aya za Surah Abasa zinazosema watu wanakimbiana siku hiyo.

Abasa ni jina la sura ya 80 ya Qur'an Tukufu ambayo iko katika Juzuu ya 30 na ina aya 42.

Ni Makki na ni Sura ya 24 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Sura ya kwanza unaanza na neno “Abasa” (alikunja uso), na kwa hiyo jina la sura.

Sura inawaonya wale wanaowaheshimu matajiri kuliko wanavyowaheshimu masikini na wasio na kitu, wale wanaozingatia zaidi watu wa dunia kuliko wachamungu.

Inawakumbusha wanadamu jinsi ulimwengu huu ulivyo mdogo, na kurejea kuumbwa kwa mwanadamu kutoka kwa “tone la mbegu” au manii na utegemezi wake kabisa katika nyanja mbalimbali za maisha. Licha ya haya, Sura hii inasisitiza kwamba mwanadamu hana shukurani.

Surah Abasa inazungumzia hatua mbalimbali za uumbaji wa mwanadamu, baraka za Mwenyezi Mungu, maisha duniani, na kisha Siku ya Kiyama na nyuso zenye furaha na huzuni za waumini na makafiri siku hiyo.

Sura inaweka mkazo maalum juu ya Siku ya Kiyama. Maudhui ya Sura yanaweza kugawanywa katika makundi matano:

 

  • Kuwakemea wanaobagua baina ya tajiri na masikini katika maingiliano yao na watu.
  • Kusisitiza umuhimu wa Qur'ani Tukufu.
  • Kukosoa utovu wa shukurani wa mwanadamu kwa Mungu pamoja na baraka zote alizompa.
  • Kurejelea baadhi ya baraka ambazo Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu,
  • Kubainisha baadhi ya matukio yatakayotokea Siku ya Kiyama na hatima ya waumini na makafiri siku hiyo.

Miongoni mwa aya za ajabu katika sura hii ni zile zinazozungumzia jinsi watu wanavyokimbiana Siku ya Kiyama.

“Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, Na mamaye na babaye, Na mkewe na wanawe, Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.  (Aya za 34-37)

Kwa mujibu wa wafafanuzi wa Qur’an Tukufu, aya hizi zinaonyesha ukali wa hali na woga uliomo katika nyoyo za watu siku hiyo. Sio tu kwamba watu watasahau kuhusu wapendwa wao wa karibu siku hiyo, kwa kweli watawakimbia.

Allamaah Tabatabai anasema sababu inayowafanya watu kuukimbia undugu wao Siku ya Kiyama ni ukali wa masharti na ugumu wa siku hiyo ambao humfanya mtu ashughulikiwe na kumzuia asifikirie chochote isipokuwa kujiokoa.

captcha