IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /34

Miujiza ya Baba, Mwana ambao ni Manabii katika Sura Saba

20:00 - October 21, 2022
Habari ID: 3475968
TEHRAN (IQNA) – Miongoni mwa Mitume waliotumwa na Mwenyezi Mungu kuwaongoza watu wengine walikuwa ni baba na mwana. Miongoni mwao ni Zakariya (Amani ya Mwenyezi Mungu-AS-) na Yahya (AS), Ibrahim (AS) na Ishaq (AS), Ibrahim (AS) na Ismail (AS), na Yaqub (AS) na Yusuf (AS).

Miujiza ya mitume wawili waliokuwa baba na mwana, yaani Dawud (AS) na Suleiman (AS), imetajwa katika Sura Saba ya Qur'ani Tukufu.

Surah Saba ni sura ya 34 ya Kitabu Kitakatifu. Ni Makki, ina aya 54 na iko katika Juzuu (sehemu) ya 22 ya Qur'ani Tukufu. Ni Sura ya 58 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina Saba linatokana na aya ya 15 ya Sura. Saba (Sheba) lilikuwa ni jina la mji wa Yemen uliokuwa makazi ya watu wenye jina moja walioishi katika zama za Suleiman alipokuwa Nabii. Mtawala wao alikuwa mwanamke aliyeitwa Bilqis.

Sehemu ya Surah Saba inasimulia kisa cha Suleiman (AS) na watu wa Saba.

Kama sura zingine za Makki yaani zilizoteremshwa katika mji wa Makka, Sura Saba inajadili kanuni za imani kama Tauhidi, Utume na Siku ya Kiyama. Pia imetaja adhabu kwa wakanushaji au wanaoeneza shaka juu ya kanuni hizi.

Sura hii inalipa kipaumbele maalum suala la Siku ya Kiyama. Masuala mengine yaliyozungumziwa katika Sura ya Saba ni pamoja na: Ishara za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu na sifa zake, mijadala baina ya waliodhulumiwa na wenye kiburi Siku ya Kiyama, baadhi ya miujiza ya manabii wa Mwenyezi Mungu, hatima ya wenye kushukuru na wasio shukuru,  na kuwaalika wanadamu kutafakari baraka za Mwenyezi Mungu.

Baadhi ya miujiza iliyotajwa katika Sura hii ni ile inayohusiana na baba na mwana: Nabii Dawud (AS) na Nabii Suleiman (AS). Dawud (AS) aliyeyusha chuma, akatengeneza silaha. Pia mara moja Dawud (AS) alisoma andiko lake na kumtukuza Mwenyezi Mungu huku milima ikiungana naye kumsifu na ndege wakimzunguka.

Suleiman (AS) alikuwa na pepo na majini chini ya amri yake. Sura pia inafafanua jinsi alivyoyeyusha shaba, kutengeneza vyombo na kujenga majengo. Inasimulia zaidi kisa cha watu wa Saba na adhabu yao na pia inazungumzia kifo cha Suleiman.

Habari zinazohusiana
captcha