IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu/8

Kitabu cha kutia moyo na Kuonya

10:28 - June 21, 2023
Habari ID: 3477174
Quran Tukufu ni kitabu ambacho tangu karne nyingi zilizopita kimeanzisha mbinu za elimu.

Na umuhimu wa njia hizi za kielimu unakuwa mkubwa zaidi pale tunapotambua kuwa mafundisho ya Qur’ani Tukufu si ya wakati maalumu bali ni wa milele. Elimu ni miongoni mwa masuala makubwa katika maisha ya binadamu binafsi na kijamii. Inamsaidia mtu kuwa na tabia inayofaa katika hali tofauti na kuweza kutumia vyema vipaji  vyake na kuelekea kwenye ukamilifu. Ndiyo sababu Mwenyezi  Mungu anakazia kwamba kutoa elimu nzuri kuwa mojawapo ya waraka kuu la wazazi. Mwenyezi Mungu, ambaye ni mwema kwa kila mtu kuliko wazazi wake, kwa kweli hutumia kanuni ya elimu, Kanuni hiyo ni mbinu mbili za kutia moyo na kuonya. Mwenyezi Mungu anasema katika  Tafisi Aya ya 4 ya Surati Fussilat; Inayo Qur’ani Tukufu  habari njema na maonyo kwa watu lakini wengi wao wamepuuza na hawasikii. Kutia moyo na onyo ni mbawa mbili za ndege wa elimu. Ikiwa kuna ukosefu wa bawa moja, hakuna ndege anayeweza kuruka. Ikiwa kuna kutia moyo sana bila onyo lolote, mtu angepuuza hatari na kuishi maisha ya kujifurahisha hadi anaingia kwenye matatizo.Kwa upande mwingine, kumpa mtu maonyo mengi kutamfanya afadhaike na kuvunjika moyo na kumzuia kusonga mbele. Qur'ani Tukufu inatumia kanuni hii kuwahimiza waumini kufanya matendo mema zaidi na kuwaonya makafiri kuhusu matokeo ya dhambi na makosa yao.Hii pia ni kanuni ambayo Mtume   Mtukufu (s.a.w.w.) anaitumia na imesisitizwa na Qur'an Tukufu Tumekutuma wewe Mtume  Muhammad kwa ajili ya kutangaza habari njema na maonyo. Hutalaumiwa kwa watu wa Jahannamu inayowaka motoni Tafsiri ya Aya ya 119 ya Surati Al-Baqarah. Kwa hivyo, Qur'ani Tukufu na Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) wanaelimisha watu na wote wawili wanatumia kanuni hii. Mifano miwili ya kutia moyo na maonyo ya Qur’ani Tukufu; Mwenyezi Mungu amewaahidi wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannamu wadumu humo, inawatosha na Mwenyezi Mungu amewalaani na watapata adhabu ya kudumu na daimaTafsiri ya  Aya ya 68 ya Surati At-Tawbah. Katika Tafsiri ya  aya hii Mwenyezi  Mungu anaahidi moto wa Jahannamu kwa makafiri na wanafiki na ni kanuni ya uhakika kwamba ahadi ya Mweneyzi Mungu haitatimizwa. 2- Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini Bustani zipitazo mito kati yake na watakaa humo daima katika majumba bora ya bustani ya Janna. Kilicho muhimu zaidi kuliko haya yote kwao ni kwamba Mwenyezi  Mungu anapendezwa nao. Huko ndiko kufuzu  viziri na Zaidi. Tafsiri ya Aya ya 72 ya Surati  At-Tawbah. Waumini wanaposoma aya hizo, wanapata  moyo zaidi kutenda mema na kuwa miongoni mwa wale watakaopokea baraka hizo.

 

 

3484015

Kishikizo: kitabu
captcha