IQNA

Shakhsia katika Qur'ani Tukufu /43

Qur'ani Tukufu Inasemaje kuhusu kusulubiwa kwa Nabii Isa (AS)

17:46 - July 13, 2023
Habari ID: 3477278
TEHRAN (IQNA) – Nabii Isa au Yesu (AS) ni shakhsia maalum katika Qur'ani Tukufu na anaelezewa kuwa ni mtu ambaye alizaliwa akiwa ametakasika na akafa akiwa ametakasika na kwamba na yuko pamoja na Mwenyezi Mungu hadi atakapotokea tena mwishoni mwa wakati ili kuwaokoa wanadamu.

Isa (AS) ni nabii maalum wa Mwenyezi Mungu ambaye ana kitabu na alileta dini. Yeye ni mtu aliyetakasika, mwenye haki, na anayeheshimika ambaye ni miongoni mwa wale walio karibu sana na Mwenyezi Mungu.

Mama yake, Mariamu (SA) alishika yake mimba kwa amri ya Mwenyezi Mungu bila kuolewa. Baada ya kuzaliwa kwake, alimpeleka Misri. Isa (AS) aliishi huko kwa siri kwa miaka 12 na kisha akaenda hadi Sham kuishi katika mji uitwao Nazareti.

Isa (AS) aliteuliwa utume akiwa na umri wa miaka 30. Dhamira yake ilikuwa ni kueneza Ukristo na kuwaalika watu kwa Mwenyezi Mungu, amani, urafiki na udugu. Ndio maana Wayahudi walianza kumpinga na hata kujaribu kumuua lakini Mwenyezi Mungu akamuokoa kupitia Malaika Jibril.

Kuna maoni tofauti kuhusu hatima ya Isa (AS). Kulingana na maelezo ya kihistoria, aliuawa au alichukuliwa na Mwenyezi Mungu hadi mbinguni.

Baada ya Isa (AS) kuwaalika watu kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, viongozi wakuu wa Kiyahudi na marabi au makuhani walianza kumpinga na kupanga njama ya kumkamata. Walifanikiwa kumkamata kwa msaada wa mmoja wa masahaba zake na baada ya kesi wakamsulubisha hadi akafa.

Kuna akaunti tofauti kuhusu tukio hili. Vitabu vya historia na vitabu vya kidini vya Wayahudi na Wakristo kila kimoja kina maelezo yake ya kile kilichotokea.

Wayahudi wanaamini kwamba Yesu alikamatwa, alihukumiwa na kuteswa na kufa chini ya mateso.

Kulingana na Wakristo, alikamatwa na kuteswa hadi kufa lakini akarudi hai baada ya siku tatu na kupaa mbinguni.

Lakini kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, mtu aliyekamatwa alikuwa mtu anayefanana na Yesu au Isa. Hiyo ni kusema, mtu mwingine alihukumiwa kimakosa, aliteswa na kuuawa.

Baada ya kujifunza kuhusu njama ya Wayahudi, Isa(AS) alikwenda mbinguni kwa amri ya Mwenyezi Mungu. “Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini ." (Aya ya 157 ya Surat An-Nisaa)

captcha