IQNA

Dini

Al-Azhar ya Misri yakemea kudhalilishwa Nabii Isa (AS) katika ufunguzi wa Olimpiki ya Paris

13:28 - July 29, 2024
Habari ID: 3479199
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimelaani matukio ya kufuru wakati wa uzinduzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris ya 2024.

Katika ufunguzi  kulikuwa na onyesho la "Drag Queens" la mwanamume aliyevaa mavazi ya kike na kujikwatua na taswira ya mchoro wa “Karamu ya Mwisho,” (Last Supper) ambayo baadhi wanasema inaonyesha picha ya Nabii Isa au Yesu, (Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake-AS).

"Taswira hiyo inaonyesha Yesu Kristo (AS) katika taswira ya kuudhi inayohusisha kutoheshimu utu wake na hadhi ya juu ya Unabii, kwa njia ya kishenzi, ya kutojali ambayo inawaudhi waumini wa dini na kukiuka maadili bora ya kibinadamu,” Taasisi ya juu ya Kiislamu ya Kisunni nchini Misri ilisema katika taarifa yake siku ya Jumapili.

Al-Azhar ilisisitiza upinzani wake mkali majaribio yote ya kutoheshimu yeyote kati ya manabii wa Mwenyezi Mungu, taarifa hiyo iliongeza.

Manabii na Mitume ni bora katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Aliwachagua na akawapendelea kuliko viumbe vingine vyote ili kupeleka ujumbe wa wema kwa walimwengu,” taarifa hiyo ilisema.

Al-Azhar, na karibu Waislamu bilioni mbili nyuma yake, wanaamini kwamba Yesu (AS) ni Mjumbe wa Allah. Qur’ani Tukufu inasema:  "Hakika Masihi Isa (Yesu) mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake.” (4:171),” taarifa hiyo iliendelea.

Mwenyezi Mungu pia amemtaja Yesu katika Qur'an Tukufu kama "mtukufu duniani na Akhera, "Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu)."

Waislamu wanaamini kwamba kutomheshimu Yesu (AS) au Mtume mwingine yeyote ni dhambi na aibu kwa wahusika wa unyanyasaji huu mbaya na wale wanaoukubali.

Al-Azhar alionya dhidi ya hatari ya kutumia vibaya matukio ya kimataifa "kufayana yawe ya kawaida matusi" kwa dini na kukuza ushoga na watu waliobadili jinsia.

3489271

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al azhar nabii isa
captcha