Kauli hizi, zilizotayarishwa kwa ustadi kwenye kibao kizuri na cha kupendeza na Taasisi ya Utafiti wa Utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu na kutafsiriwa kwa Kiitaliano, ziliwasilishwa na Dk. Mohammad Hossein Mokhtari, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Vatican, wakati wa mkutano wa ana kwa ana na Papa Francis hivi karibuni.
Papa alipokea kwa uchangamfu kibao hicho, akieleza shukrani zake za dhati. Alisisitiza kuwa kibao hiki kina pointi muhimu na maarufu ambazo zinaweza kuwa na athari na ushawishi mkubwa kwa wafuasi wa imani ya Kikristo.
Wakati wa mkutano huu, Papa Francis alielezea wasiwasi wake kuhusu hali katika eneo la Asia Magharibi, hasa vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Palestina. Amesisitiza kuwa anafuatilia taarifa za kila siku kuhusu hali na matukio katika eneo hilo kupitia mwakilishi wake nchini Palestina.
Mwisho wa mkutano huu, Papa Francis alimuomba Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Vatican kufikisha salamu zake za upendo kwa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Nakala ya kibao hiki, ambayo imetafsiriwa kwa Kiitaliano, ni kama ifuatavyo:
Ikiwa Kristo angekuwa miongoni mwetu…
Umuhimu wa Nabii Isa (Amani ya Iwe Juu Yake) machoni mwa Waislamu bila shaka ni sawa na umuhimu na heshima aliyo nayo machoni mwa Wakristo wacha Mungu. Nabii huyu mkuu wa Mwenyezi Mungu alitumia wakati wake wote miongoni mwa watu katika mapambano ili kukabiliana na dhuluma, uchokozi na ufisadi, pamoja na kukabiliana na wale waliokuwa wakitumia utajiri na nguvu zao kuyafanya mataifa kuwa watumwa na ikiwa angekuwepo leo angewapeleka katika jahanamu ya dunia hii na ya akhera.
Inatarajiwa kwamba wafuasi wa Yesu Kristo na wote wanaotambua ukuu wake na umaanawi wake wa kina, ambao unaendana na hadhi yake ya juu, watamfuata katika njia hii.
Kama Yesu (Amani ya Iwe Juu Yake) angekuwa miongoni mwetu hii leo, asingesitasita hata kidogo kupambana na viongozi wakandamizaji na mabeberu wa dunia ya leo, na wala asingestahamili njaa na kulazimishwa kuhama kwa mabilioni ya watu ambao wamesukumwa vitani na madola ya kibeberu.
Leo, Wakristo na Waislamu wote wanaomuamini Nabii huyu mkuu lazima waelekee kwenye mafundisho na njia za mitume na manabii wa kweli wa Mwenyezi Mungu ili kuanzisha mfumo wa haki ulimwenguni. Lazima waendeleze maadili ya kibinadamu kama yanavyofundishwa na walimu hawa wa ubinadamu.
Kuwa mfuasi wa Yesu Kristo au Nabii Isa (Amani ya Iwe Juu Yake) kunamaana ya kuuwa ni lazima utetee ukweli na kukataa nguvu zinazoupinga. Inatarajiwa kwamba Wakristo na Waislamu katika pembe zote za dunia wataendeleza somo hili la kina la Nabii Isa (Amani ya Iwe Juu Yake) katika maisha yao na matendo yao.
Chanzo: Khamenei.ir
3491333