IQNA

Mawaidha

Nabii Isa (AS) katika Qur'ani Tukufu

20:40 - December 29, 2023
Habari ID: 3478107
IQNA – Nabii Isa au Yesu (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-) ni miongoni mwa Manabii Ulul'adhm (manabii wakuu) na kitabu chake ni Biblia.

Alikuwa mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu kabla ya Mtume Muhammad (SAW).

Uchunguzi wa aya za Qur'ani Tukufu kuhusu Isa (AS) unaonyesha kwamba aya za Mwenyezi Mungu zinazungumza kuhusu kisa cha kuzaliwa kwake, utakatifu wa mama yake Maryam (SA), na kuzungumza kwake utotoni, miongoni mwa nyinginezo.

Baadhi ya aya zinaelekeza kwa wanafunzi wake 12 na Aya ya 55 ya Sura Al Imran inakataa wazo la kusulubiwa kwake: “Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana."

Kwa ujumla, jina Isa limetajwa katika Qur'ani Tukufu mara 25, Masihi mara 11, na ‘Mwana wa Mariamu’ mara 23.

Kinyume cha yale ambayo yemepotoshwa katika Bibilia, Nabii Isa katika Uislamu si  mwana wa Mungu bali mtumishi wa Mungu.

“(Isa akasema): Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.” (Aya ya 117 ya Surah Al-Ma’idah)

3486552

Kishikizo: nabii isa
captcha