IQNA

Jinai za Israel

Walowezi na askari katili wa Israel waua Mpalestina 1, na kujeruhi wengine 18

13:02 - July 20, 2023
Habari ID: 3477310
Al-QUDS (IQNA) - Vikosi vya utawala wa Kizayuni na walowezi haramu walivamia mji wa Nablus katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan mapema Alhamisi na kumuua Mpalestina mmoja na kujeruhi wengine wasiopungua 18.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Shihab, mamia ya walowezi  wa Kizayuni walivamia kaburi la Yusuf (AS) katika eneo la mashariki mwa mji huo chini ya ulinzi wa majeshi ya Kizayuni.
Vijana wa Kipalestina na wapiganaji wa upinzani walikabiliana na vikosi vya uvamizi na walowezi, jambo ambalo lilisababisha mapigano.
Vikosi vya  utawala haramu wa Israel viliwafyatulia risasi Wapalestina na mabomu ya machozi, ripoti hiyo ilisema.
Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Palestina ilisema kwamba vikosi vya uvamizi vimempiga risasi Mpalestina na kuwajeruhi wengine wanne - wawili kati yao katika hali mbaya.
Imeongeza kuwa Wapalestina 15 pia walitibiwa kwa kuvuta gesi ya kutoa machozi.
Mpalestina aliyeuawa shahidi katika mapigano hayo ni Badr Sami Raihi Misri ambaye alipigwa risasi kifuani na baadaye kufariki akiwa hospitalini.
Kikosi cha Nablus cha Brigedi ya al-Quds, tawi la wanaharakati wa harakati ya Jihad ya Kiislamu, kilisema wanachama wake "walikuwa wakipambana na vikosi vya uvamizi na vikundi vya walowezi ambao walivamia eneo la Kaburi la Joseph." 
Walowezi wa Israel kila kukicha huvamia na kuchafua maeneo matakatifu katika miji ya Al-Quds na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan chini ya ulinzi wa majeshi ya Kizayuni, hivyo kuibua hisia za Wapalestina.

Kwingneko, duru za habari za Palestina zimetangaza kuwa, wanamapambano wa Palestina jana walitekeleza oparesheni 20 za kimuqawama dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.

Wazayuni hushambulia maeneo mbalimbali ya Palestina na kuwaua shahidi, kuwajeruhi, kuwatia mbaroni na kuwafunga jela raia wa Palestina wasio na hatia; ambapo Wapalestina pia katika kujibu jinai hizo hutekeleza oparesheni mbalimbali dhidi ya Wazayuni hao maghasibu. Wazayuni wanatekeleza jinai zote hizi ili kufikia malengo yao ya kujitanua huko Palestina.  

Shirika la habari la Mehr limeripoti kuwa, Kituo cha Takwimu za Palestina cha Maati kimetangaza kuwa oparesheni hizo zinajumuisha matukio mawili ya ufyatuaji risasi, kuchomwa moto mnara wa kituo cha ulinzi cha Israel, kukabiliana na mashambulizi ya walowezi wa kizayuni na kujiri mapigano 12 kati ya wanamuqawama na wanajeshi wa Israel. 

Mwanajeshi mmoja na walowezi watano wa Kizayuni wamejeruhiwa katika oparesheni hizo za kimuqawama za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi.  

Wakati huo huo, katika tukio jingine huko Palestina, walowezi kadhaa wa Kizayuni leo wameuvamia msikiti wa al Aqsa huku wakisindikizwa pakubwa na wanajeshi wa Kizayuni. Walowezi hao wameingia msikitini hapo kupitia lango la Bab al Maghriba. 

 
4156493

captcha