IQNA

Uislamu na Teknolojia

Apu mpya ya kufundisha watoto Qur’ani yazinduliwa Saudi Arabia

20:04 - December 18, 2023
Habari ID: 3478054
IQNA-Jumuiya ya Kuhudumia Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Al-Burhan imezindua apu mpya iliyopewa jina la Salim inayowasaidia watoto walio na umri wa chini ya miaka 8 kujifunza Quran bila ya kuhitaji mwalimu.

Uundaji wa apu hiyo umefadhiliwa na Wakfu wa Abdullah al-Raji. Aou hiyo Inachanganya michezo na mbinu za kufundishia kwa elimu ya Qur'ani.

Programu hiyo huwasaidia watoto kujifunza kusoma Qur’ani Tukufu kwa namna ya visa vya kuelimisha ambapo watoto hufuatana na Salim, mvulana mwenye akili na busara akiwa na ndege wake, katika safari.

Wanapitia hatua mbalimbali, ambazo huwa ngumu kupita kadri safari inavyoendelea, ili kurudisha masanduku ya nuru yaliyoibiwa na viumbe wa kishetani.

Safari inapoendelea, watoto, kupitia michezo ya kufurahisha na kuburudisha, hujifunza jinsi ya kutamka kwa usahihi maneno ya Sura za Qur’ani Tukufu.

Teknolojia na programu mbalimbali mpya, ikiwa ni pamoja na zana za utambuzi wa usemi zinazoendeshwa na Akili Mnemba au Artificial Intellligence AI, zimetumika kutengeneza apu hii

Abdul Rahman bin Khazir al-Khazir, afisa wa Jumuiya ya Kuhudumia Quran na Sunnah ya Al-Burhan, alisema wazo la kuunda apu ya aina hiyo liliibuliwa baada ya jamii kutambua hitaji la familia za Kiislamu kuwa na programu inayofundisha Quran kwa watoto kwa njia rahisi.

 

4188553

Kishikizo: apu qurani tukufu saudia
captcha