IQNA

Ahul Bayt (AS)

Haram ya Imam Ali (AS) imeandaa vikao vya Qur'ani katika maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (SA)

18:44 - January 02, 2024
Habari ID: 3478134
IQNA - Idadi kadhaa ya maqari au wasomaji Qur'ani Tukufu kutoka Iraq na nchi nyingine watashiriki katika programu ya usomaji wa Qur'ani Tukufu katika Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) huko Najaf, Iraq.

Usomaji huo wa Qur'ani Tukufu utafanyika katika hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bibi Fatima Zahra (SA), mke wa Imam Ali (AS).

Vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu  ni sehemu ya tamasha la Ifaf lililoanza kwenye Haram Takatifu ya Imam Ali (AS) siku ya Jumatatu,

Haidar Rahim, mkuu wa ofisi ya vyombo vya habari ya Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali (AS) alisema tamasha hilo litaendelea kwa wiki moja.

Rahim aliongeza kuwa maprofesa kadhaa wa kike wa vyuo vikuu na walimu wa shule na wanafunzi pia watatunukiwa kwa mafanikio yao.

Siku ya 20 ya mwezi wa Jumada al-Thani katika kalenda ya mwandamo ya Hijria Qamaria, ambayo mwaka huu  inaadhimishwa Jumatano, Januari 3, mwaka huu, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa binti kipenzi cha Mtume Mtukufu (SAW), Bibi Fatima Zahra (SA).

Siku hii inaadhimishwa kama Siku ya Wanawake na Siku ya Mama nchini Iran na katika jamii nyingi za Waislamu duniani kote.

3486648

captcha