IQNA

Mkutano wa Qur’ani Tukufu Diyala, Iraq Wajadili Hadhi ya Bibi Zahra (SA)

19:22 - November 28, 2025
Habari ID: 3481583
IQNA-Mkutano wa kielimu wa Qur’anI Tukufu uliopewa jina “Bibi Fatima Zahra (SA) na Sheria za Uteuzi wa Kimaumbile” umefanyika katika jimbo la Diyala, Iraq ukiratibiwa na Jumuia ya Kisayansi ya Qur’an chini ya usimamizi wa Haram ya Abbas (AS).

Miongoni mwa wazungumzaji alikuwa mwanazuoni Sayyid Sajjad Al-Askari, aliyebainisha dhana ya sheria za uteuzi wa kimaumbile katika Qur’ani Tukufu, akieleza maana yake ya kifasaha na ya Qur’ani. Alitoa mifano ya uteuzi wa Mwenyezi Mungu, ikiwemo uteuzi wa Bibi Maryam (SA) kuwa mama wa Nabii Isa (AS) kutokana na hadhi yake ya kiroho na ibada zake.

Mkutano huo pia uliangazia nafasi ya Bibi Zahra (SA) kama kiungo safi cha Utume na Uimamu, na jinsi Maimamu (AS), akiwemo Imam Mahdi (Allah aiharakishe kudhihiri kwake), walivyoteuliwa kutoka miongoni mwa kizazi chake. Al-Askari pia aligusia dhulma na mateso aliyoyapata Bibi Zahra (SA).

Hii ni sehemu ya mfululizo wa mikutano na programu zinazoandaliwa na Jumuia ya Kisayansi ya Qur’ani katika mikoa mbalimbali ya Iraq, kwa lengo la kueneza utamaduni wa Qur’ani na kuongeza uelewa kuhusu hadhi ya Ahlul-Bayt (AS).

3495540

Habari zinazohusiana
captcha