IQNA

20:25 - February 26, 2019
News ID: 3471854
TEHRAN (IQNA). Sherehe za Mazazi ya Bibi Fatima Zahra SA hivi karibuni zimewaleta pamoja Waislamu na wapenzi wa Ahul Bayt wa Mtume SAW katika katika Markaz Mafaatihul Jinaan, Kiguza, Mkuranga, Pwani nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Majlisi hiyo iliyofana iliwavutia wanawake na wasichana wa matabaka mbali mbali ambao walisikiliza qaswida na mawaidha kumhusu Bibi Fatima Zahra SA.

Leo, Jumanne tarehe 20 Mfunguo Tisa Jumadithani 1440 Hijria sawa na Februari 26, mwaka 2019 Milaadia inasadifiana na kumbukumbu ya mazazi ya Bibi Fatima Zahra SA.

Itakumbukwa kuwa siku kama ya leo miaka 1448 iliyopita, alizaliwa Bibi Fatima Zahra, binti mtukufu wa Mtume Muhammad SAW. Bibi Fatima Zahra alilelewa katika nyumba ya wahyi na chini ya malezi bora na mwongozo wa baba yake Mtume Muhammad SAW na hivyo kuweza kufikia daraja za juu za ukamilifu. Bibi Fatima (as) alikuwa na nafasi kubwa katika kukabiliana na matatizo na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikimkabili baba yake kutoka kwa washirikina. Mwaka wa pili Hijiria, Bibi Fatima Zahra alifunga ndoa na Imam Ali bin Abi Twalib AS ambaye ni dhihirisho la haki, uadilifu na uchaji-Mungu katika sherehe ndogo iliyosimamiwa na Mtukufu Mtume Muhammad (saw). Vilevile Bibi Fatima akiwa na Imam Ali alifanikiwa kulea shakhsia adhimu kama Hassan, Hussein na Bibi Zainab AS . Mbali na majukumu ya kulea familia, Bibi Fatima Zahra, alijishughulisha pia na malezi ya jamii.

Hapa chini ni baadhi ya picha za sherehe za Mazazi ya Bibi Fatima Zahra SA huko Mkuranga Tanzania.

Majlis ya Mazazi ya Bibi Fatima Zahra SA, Mkuranga Tanzania

3793496

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: