IQNA

Wasomi Waislamu

Mkuu wa ACECR asisitiza utafiti wa maoni ya Kiongozi Muadhamu kuhusu Dkt. Ashtiani

22:00 - January 05, 2024
Habari ID: 3478152
IQNA - Rais wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) ameisitiza haja ya kuchunguza maoni ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu marehemu mwanasayansi wa Iran Dakta Saeid Kazemi Ashtiani.

Akihutubu  katika hafla iliyofanyika katika Makaburi ya Behesht Zahra mjini Tehran siku ya Alhamisi ya kumkumbuka Dakta Kazemi Ashtiani katika kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo chake, Hassan Moslemi Naeini alisema yeye mwenyewe alijifunza kuhusu mwanazuoni huyo mashuhuri na kazi zake kupitia matamshi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei.

Pia alihimiza kila mtu kusoma vitabu viwili vilivyoandikwa kuhusu maisha na shughuli za Dkt. Kazemi Ashtiani.

Dk Kazemi Ashtiani ni mfano wa kuigwa kwa kila mtu kwani wasomi, wafanyakazi, madaktari na wengine wanaweza kufaidika kutokana na kujifunza kuhusu maisha na matendo yake, alisisitiza.

Moslemi Naeini alisema moja ya sehemu kuu ya tamko la Awamu ya Pili ya mapinduzi ni kuhusu mambo ya kiroho na maadili na hayo ni miongoni mwa maeneo ambayo Kazemi Ashtiani ilifahamika.

Pia alibainisha kwamba Kazemi Ashtiani aliipenda Qur'ani Tukufu na alikuwa msomaji wa Qur'ani na alikuwa amehifadhi aya nyingi za Kitabu hicho Kitakatifu.

Kwingineko katika matamshi yake, mkuu wa ACECER alilaani shambulizi la kigaidi lililoua karibu watu 100 katika mji wa Kerman kusini mwa Iran siku ya Jumatano na kuwatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa katika shambulio hilo. Ameongeza kuwa, hatua hizo za maadui zinaimarisha tu Mapinduzi ya Kiislamu.

Kando ya hauli hiyo, maonyesho yaliyopewa jina la "Saeid wa Iran" yaliandaliwa kwenye Makaburi ya Behesht Zahra kuhusu maisha na mafanikio ya Dk Kazemi Ashtiani.

Dk Kazemi Ashtiani alikuwa mwanzilishi katika uwanja wa utafiti wa seli shina na mwanzilishi wa Taasisi ya Utafiti ya Royan.

Kulingana na tovuti ya Taasisi ya Royan, Dk Saeid Kazemi Ashtiani alizaliwa Machi 1961 huko Tehran. Alipomaliza shule yake ya upili akiwa na umri wa miaka 18, alilazwa katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Iran ili kuendeleza masomo yake katika fani ya Tiba ya viungo.

Alihitimu mwaka wa 1991 na baadaye mwaka wa 1993 alianza elimu yake ya juu katika fani ya Anatomia (tawi la Embryology) katika Chuo Kikuu cha Tarbiat Modaress huko Tehran. Mnamo 1998, alipata Shahada ya Uzamivu ya ngazi za juu.

محسن قلی پور، معاون پژوهشی جهاددانشگاهی

Dk Kazemi alianzisha Taasisi ya Utafiti ya Royan mnamo 1991.

Dk Kazemi na wenzake katika Kituo cha Utafiti wa Utasa cha Royan waliweza kupata mafanikio makubwa mwaka wa 2003 kwa kuzalisha seli shina. Ugunduzi huu mkubwa wa kisayansi ulipelekea Iran kuwa kati ya nchi zingine 10 bora zinazoweza kupata teknolojia hii ya hali ya juu ya seli shina.

Aliwahi kuwa Mkuu wa ACECR, Tawi la Chuo Kikuu cha Tiba cha Iran, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Royan, mwalimu mgeni na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Iran pamoja na Chuo Kikuu cha Shahid Beheshti, meneja Mtendaji wa uzalishaji wa mradi wa seli shina katika Taasisi ya Utafiti ya Royan, mhariri mkuu wa Jarida la Sayansi na Utafiti la Yakhteh, Mkuu wa Kamati ya Matatizo ya Kimaadili katika Taasisi ya Royan, mwanachama hai wa Jumuiya ya Ugumba ya Iran na Jumuiya ya Sayansi ya Anatomia ya Iran.

Dk Saeid Kazemi pia aliongoza Tuzo la Kimataifa la Royan, lililofanyika mara sita kutoka 2000-2005. Maisha yake mafupi yaliyojaa faida kwa jamii ya mwandamu yaliisha mwaka wa 2006 alipofariki kutokana na mshtuko wa moyo wa ghafla.

3476479

Kishikizo: ACECR
captcha