IQNA

Mkutano kuhusu Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi wa Kiislamu

21:08 - August 12, 2024
Habari ID: 3479268
IQNA – Maafisa wa Makao Makuu ya Uratibu wa Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Iran yalifanya mkutano siku ya Jumamosi mjini Tehran.

Ajenda kuu ya  mkutano huo ilikuwa ni kuhusu maandalizi ya toleo la 7 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi wa Kiislamu, amebaini Hamid Majidimehr, katibu wa makao makuu.

Aliiambia IQNA kuwa wakuu wa kamati za makao makuu na wajumbe wake walikuwepo kwenye kikao hicho.

Alisema baada ya majadiliano  kwamba pande husika zisaidie Shirika la Qur'ani la Wanataaluma wa Iran, linaloshirikiana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR), kuandaa tukio hilo la kifahari la Qur'ani.

Majidimehr ameeleza matumaini yake kuwa wawakilishi wa kidiplomasia na kiutamaduni wa Iran katika nchi mbalimbali duniani pia wataisaidia jumuiya hiyo katika kubainisha na kuwaalika watu wenye vipaji vya juu vya Qur'ani kushiriki katika mashindano hayo.

Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran imekuwa ikiandaa mashindano hayo tangu mwaka 2006 kwa lengo la kustawisha umoja na ushirikiano kati ya wanafunzi wa ulimwengu wa Kiislamu na kuinua kiwango cha shughuli za Qur'ani.

3489456

Habari zinazohusiana
captcha